BREAKING NEWS

Friday, April 22, 2016

SAMIA AZITAKA NCHI ZA MAZIWA MAKUU KUHAKIKI NA KUWEKA ALAMA SILAHA ZILIZOKO MIKONONI MWA WATU

Na Woinde Shizza,Arusha

 MAKAMU wa Raisi wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania Samia

Suluhu    amewataka mawaziri wa mambo ya ndani wa nchi za maziwa makuu
kuhakiki na kuweka alama silaha zilizopo mikononi  kwa watu  ili
kuweza kupunguza uhalifu  na uvunjifu wa amani wan chi hizo.

Hayo aliyasema jana (leo)wakati akifungua mkutano wa nane  wa taasisi
inayojishulika na uthibiti wa silaha ndogo  na za kati ambazo nyingi
zipo mikononi mwa watu na zinamilikiwa na watu binafsi  (RECSA)
uliowashirikisha  mawaziri wa mambo ya ndani wanchi 15 za afrika.

Alisema kuwa ni muhimu nchi za afrika kuakikisha wanahakiki  na kuweka
alama silaha zilizopo mikononi mwa watu ambapo hii itasaidia  kutambua
kwa haraka silaha inamilikiwa na nani pamoja na kuonyesha silaha
imetokea nchi gani.

“sisi kwa Tanzania tumeshaanza kuakiki silaha zetu na zoezi hili
liliongozwa na rais wetu John Magufuli sasa hizi nchi zingine ambazo
azijaanza swala hilo naomba waanze kwani kuhakiki huku kutasaidia sana
kupunguza maswala ya uhalifu wa silaha pamoja na kuondoa kabisa
kabisa vita vya wananchi ambao wanatumia silaha”alisema Samia

Alisema kuwa iwapo silaha hizi zikiwekwa alama itakuwa rais iwapo
silaha ikikamatwa kujulikana ni nani anaimiliki na pia kama sio ya
nchi husika itakuwa rahisi kujua imetoka nchi gani na ili iweze
kuchukuliwa hatua .

Aidha pia Makamu wa Rais aliitaka jumuiya hii kuwapa wanawake
kipaumbele kwa kuwaweka katika mikutano hiii kwani japo kuwa hawezi
kwenda kupigana vita lakini wataweza kuangalia jinsi ya kuleta amani
ya nchi .

“unajua najua wanawake hatuwezi kwenda kupigana vita lakini katika
swala la kuleta amani tunaweza hata kwa kuchangia mada na pia hata kwa
kushauri hivyo naomba wanawake wapewe kipaumbele kwa kweli”alisema
Samia

Aidha aliwataka mawaziri hao  wanaoendelea na mkutano kujadili maamuzi
ya nini kifanyike ili kupunguza silaha nyingi ambazo zipo mikononi mwa
watu kwani zimekuwa zikichangia kuwepo kwa vita na pia silaha hizo
zinazuia maendeleo iwapo vita itatokea

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates