BREAKING NEWS

Thursday, April 28, 2016

PROGRAMU YA FURSA KWA WATOTO YAZINDULIWA DAR,LENGO IKIWA NI KUBORESHA ELIMU YA AWALI

Programu ya Fursa Kwa Watoto yazinduliwa Dar, lengo kuboresha elimu ya awali
_MG_9991
Na Rabi Hume


Kwa kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto ambao ndiyo watakuja kuwa viongozi wa baadae nchini, programu mpya inayofahamika kama Fursa Kwa Watoto imezinduliwa leo ikiwa na malengo ya kuboresha elimu kwa watoto wanaoanza elimu ya awali ili kuwafanya kuwa na uwezo pindi wanapoanza elimu ya shule ya msingi.
Akizungumzia programu hiyo, Mratibu wa Elimu ya Awali kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo, Clarence Mwinuka amesema kuwa kabla ya kuletwa kwa programu hiyo kulikuwa na matatizo ambayo yakikabili elimu ya awali hivyo kuwafanya wanafunzi wanaomaliza elimu hiyo kutokuwa na uwezo wa kutosha kuanza elimu ya msingi.
Amesema kupitia programu hiyo ambayo kwa kuanzia itafanyika Mwanza na Moshi ambapo itafanyika kwa miaka miwili na baada ya hapo watawachunguza watoto hao kama watakuwa wamekuwa na uwezo wa kutosha kwa ajili ya kujiunga na elimu ya msingi.
“Kila mtoto anatakiwa kuanzia elimu ya awali na kupitia programu hii walimu watapewa mafunzo, vifaa vitatolewa na kuwatengenezea mazingira mazuri ya kuwapa motisha alafu baada ya programu kumalizika tutaona matokeo yakoje,” amesema Mwinuka.
DSC_0902
Mratibu wa Elimu ya Awali kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo, Clarence Mwinuka akizungumzia hali ya elimu ya awali ilivyo nchini na mafanikio yanayoweza kupatikana kutokana na programu hiyo. (Picha zote na Rabi Hume wa MoDewjiBlog)
Nae Mtendaji Mkuu wa Dubai Cares ambao dhiyo wadhamini wa programu hiyo, Tariq Al Gurg amesema wameamua kudhamini programu hiyo nchini ili kusaidia kukuza elimu nchini.
Amesema Falme za Kiarabu imekuwa nchi ambayo inashirikiana na Tanzania katika mambo mbalimbali na hivyo wanaamini programu hiyo itakuwa na matokeo mazuri na kuwafanya wanafunzi wanaoingia kuanza elimu ya msingi kuwa na uwezo wa kutosha.
“Tumesaidia programu hii ili kuboresha elimu ya Tanzania ambayo itafanyika mpaka 2018, tuna tumaini itafanikiwa,” amesema Gurg.
DSC_0822
Mtendaji Mkuu wa Dubai Cares, Tariq Al Gurg akizungummzia udhamini wao kwa programu hiyo na matarajio yao. Kushoto ni Meneja Programu wa Dubai Cares, Saeed Alissmaily.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Shirika la Crossfire nchini ambayo inahusika maendeleo ya elimu kwa watoto, Graig Ferla amesema ni jambo zuri kuwekeza katika elimu ya watoto kwa ajili ya matokeo mazuri ya baadae kwa kuanzia darasani hadi katika maisha ya kawaida.
DSC_0862
Mkurugenzi wa Shirika la Crossfire nchini, Graig Ferla akizungumzia jinsi programu hivyo inaweza kufanikiwa nchini na umuhimu wa kuwekeza katika elimu kwa kuanza na elimu ya awali. Kulia ni Meneja Programu wa Dubai Cares, Saeed Alissmaily na Mtendaji Mkuu wa Dubai Cares, Tariq Al Gurg
DSC_0878
Mkuu wa Elimu kutoka Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Cecilia Baldeh akizungumzia umuhimu wa kuwa na mipango wa kuboresha elimu nchini hasa kutokana na kuwa na waziri ambaye yupo tayari kuona hilo likifanyika. Kushoto ni Mratibu wa Elimu ya Awali kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo, Clarence Mwinuka na Mtendaji Mkuu wa Dubai Cares, Tariq Al Gurg.
_MG_9991
Uzinduzi wa programu ya Fursa Kwa Watoto ukifanyika.
DSC_0899
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka Tanzania na Falme za Kiarabu (UAE) waliohudhuria mkutano wa uzinduzi wa programu hiyo.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates