WABUNGE WATAKA TANESCO ITUMBULIWE MAJIPU


 Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara Mbunge wa Arusha mjini
Godbless Lema na Vicky Kamata wakisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja
uzalishaji wa kiwanda cha Tanalec Michael Laizer jana walipotembelea
kiwanda hicho kilichopo jijini Arusha



Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara ,watatu kushoto
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dalali Kafumu,Mbunge wa Arusha mjini Godbless
Lema na Vicky Kamata wakisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja uzalishaji wa
kiwanda cha Tanalec Michael Laizer jana walipotembelea kiwanda hicho
kilichopo jijini Arusha.



 Na Woinde Shizza,Arusha
 
Wabunge wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambao ni Wajumbe wa Kamati
ya Viwanda na Biashara wamemtaka Rais John Pombe Magufuli kulitumbua
jipu shirika la umeme Tanesco kwa kununua transfoma kutoka nje ya nchi
licha ya kumiliki asilimia 20% ya hisa katika kiwanda cha Tansfoma cha
Tanalec kilichopo jijini Arusha .



Kamati hiyo ya Bunge imebaini hayo   wakati wa ziara yao ya kutembelea
viwanda jijini Arusha ili kufahamu changamoto na kasi ya ukuaji wa
viwanda ambapo Wabunge hao wameshangazwa na kitendo cha Tanesco
kutonunua transfoma katika kiwanda hicho ambazo huuzwa katika nchi
jirani za Kenya ,Zambia Malawi na Burundi.



Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ambaye ni Mjumbe wa Kamati hiyo
alisema kuwa ni jambo la kushangaza kwa Tanesco ambao ni wamiliki wa
Tanalec na wako katika wakurugenzi wa bodi lakini bado wanaagiza
transfoma nje ya nchi suala ambalo linapaswa kutazamwa kwa umakini na
kupatiwa majibu.



“Tunashindwa kuilewa Tanesco kwanini wanafanya hivyo wakati kiwanda ni
cha kwao  na wakati Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco  Felchesmi Mramba  yuko
ndani ya bodi ya wakurugenzi ,hapa kuna mgogoro ambao unapaswa
kuatatuliwa kwa wakati ili kunusuru kiwanda hiki” Alisema Lema



Naye Mbunge wa Singida Mjini Musa Sima wamesema kuwa uamuzi huo wa
Tanesco kununua  transfoma za nje ya nchi unazorotesha ukuaji wa
viwanda vya ndani na kukiuka adhma ya Rais Magufuli ya kujenga uchumi
wa viwanda nchini kwani ni vigumu kukuza viwanda wakati bila kuvilinda
viwanda vya ndani dhidi ya bidhaa za nje.





Makamu Mwenyekiti wa  Kamati hiyo Vicky  Kamata  na Mwenyekiti wa
Kamati hiyo Dalali Kafumu wameitaka serikali kuchukua maamuzi juu ya
suala hilo la Tanesco ili kulinda viwanda vya ndani viweze kuchochea
maendeleo ya Taifa.





Meneja Mkuu  wa Tanaleck Zahir Salehe ameiomba serikali irekebishe
sheria za manunuzi ili zitoe kipaumbele kwa viwanda vya ndani viweze
kukua na kutoa ajira nyingi hivyo kukuza pato la nchi.


Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post