BREAKING NEWS

Tuesday, April 26, 2016

HOSPITALI YA NGARENARO YAKABILIWA NA UHABA WA VIFAA TIBA





Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki
Ruth Mtoi Simba akikabidhi msaada  wa vifaa tiba kwa  Muuguzi Mkuu wa
Hospitali ya Ngarenaro  Hosea Naaman ,msaada uliotolewa na Umoja wa
Watanzania wanaofanya kazi katika jumuiya ya Afrika Mashariki  maarufu kama
(WATJAM)jana jijini Arusha.




Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki
Ruth Mtoi Simba akikabidhi msaada  wa vifaa tiba kwa  Muuguzi Mkuu wa
Hospitali ya Ngarenaro  Hosea Naaman ,msaada uliotolewa na Umoja wa
Watanzania wanaofanya kazi katika jumuiya ya Afrika Mashariki  maarufu kama
(WATJAM)jana jijini Arusha.



 Na Woinde shizza,Arusha.

Hospitali ya Ngarenaro iliyoko wilaya ya Arusha mjini mkoa wa Arusha
inakabiliwa na uhaba wa vifaa tiba pamoja na ukosefu wa miundombinu ya
maji katika wodi ya wazazi jambo ambalo linapunguza ufanisi wa
upatikanaji wa huduma za afya kwa wagonjwa.

Muuguzi Mkuu wa Hospitali hiyo Hosea Naaman  amesema kuwa uchache wa
vifaa tiba umekua ukiathiri ari ya wauguzi katika kuwahudumia wagonjwa
licha ya juhudi zinazofanywa na serikali bado hospitali hiyo ina
mahitaji ya vifaa tiba hasa katika wodi ya wajawazito



Kufuatia Changamoto hizo Umoja wa Watanzania wanaofanya kazi katika
jumuiya ya Afrika Mashariki  maarufu kama (WATJAM) wameitikia wito na
kujibu changamoto hizo kwa kutoa msaada wa vifaa tiba mbalimbali
ikiwemo gloves,mashuka,ambavyo vitawezesha upatikanaji wa huduma bora
kwa mama na mtoto.

Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu Ruth Mtoi Simba amesema kuwa
Watanzania wanaofanya kazi katika jumuiya wameamua kuchangia huduma za
kijamii ili kuwasaidia watanzania wenye kipato cha chini kupata huduma
bora za afya

Mwanachama wa  Umoja huo  Fadhili Mganya na Katibu wake Costantini
Mashauri wamesema kuwa umoja huo umelenga kuwasaidia watanzania
kutatua changamoto mbalimbali za afya ,kijamii na kiuchumi kwa
kushiriki katika kutatua changamoto hizo

Umoja wa Watanzania wanaofanya kazi katika jumuiya ya Afrika Mashariki
leo wamesheherekea sikukuu ya Muungano kwa kutembelea hospitali ya
Ngarenaro na kutoa msaada wa vifaa tiba ili kusaidia kuboresha huduma
za afya .

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates