Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja
na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakifurahia mara baada ya kuzindua
rasmi daraja
hilo la kimataifa la Rusumo na Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani
(OSBP) cha Rusumo. Tukio hilo limehudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu
serkalini kutoka Nchi zote mbili, Mabalozi, na Viongozi wa Taasisi
mbambali za Kitaifa na Kimataifa.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja
na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakikata utepe kwa pamoja kuashiria
uzinduzi rasmi wa daraja la kimataifa la Rusumo na Kituo cha Huduma kwa
Pamoja
Mpakani (OSBP) cha Rusumo. Tukio hilo limehudhuriwa na viongozi wa ngazi
za juu
serkalini kutoka Nchi zote mbili, Mabalozi, na Viongozi wa Taasisi
mbambali za
Kitaifa na Kimataifa.
Ujenzi
wa Daraja la Kimataifa la Rusumo na Kituo cha huduma Pamoja Mpakani Rusumo ni
moja ya miradi inayotekelezwa kwa msaada kutoka Serikali ya Japan kwa Nchi za
Tanzania na Rwanda kupitia shirika lake la maendeleo la JICA. Mradi huu kwa
upande wa Tanzania umegharimu takribani kiasi cha TShs. 33,206,508,072.07 hadi
kukamilika. Miradi mingine inayotekelezwa kwa kushirikiana na Serikali ya Japan
kupitia JICA ni pamoja na ujenzi wa Barabara ya Arusha – Namanga, Iringa –
Dodoma, Namtumbo – Kilimasera – Matemanga – Tunduru pamoja na barabara ya
Masasi - Mangaka.
Muonekano wa sehemu ya Daraja hilo la Rusumo
Jiwe la msingi lililowekwa baada ya uzinduzi wa daraja hilo
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja
na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakipita kwenye Daraja hilo la Rusumo
mara baada ya uzinduzi
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja
na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakikata utepe kwa pamoja kuashiria
uzinduzi Kituo
cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Rusumo. Tukio hilo
limehudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu serkalini kutoka Nchi zote
mbili, Mabalozi, na Viongozi wa Taasisi mbambali za Kitaifa na
Kimataifa.
Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa huo