SEREKALI YATAKIWA KUKUMBUKA MAHABUSU YA WATOTO ARUSHA KWANI INAKABILIWA NA CHANGAMOTO NYINGI IKIWEMO YA UKOSEFU WA DAWA NA USAFIRI KWA MAHABUSU

 katibu wa Jumuiya ya wazazi   ccm wilaya Arusha  Rehema mohamed katikati akiwa na wajumbe wengine wa Kamati ya utekelezaji Jumuia ya wazazi wilaya ya Arusha wakati walipotembelea mahabusu ya watoto iliopo ndani ya jiji la Arusha hii ikiwa ni moja ya sehemu yao ya kuazimisha sherehe ya wiki ya wazazi Tanzania
 wajumbe wakewa wanasubiri kukabidhi baadhi ya vifaa ambavyo walienda kukabidhi katika mahabusu  hiyo ya watoto
 wajumbe wakiwa wanamkabidhi Afisa ustawi wa jamii wa mahabusu ya watoto Arusha baadhi ya vitu ambavyo walivipeleka  kwa ajili ya watoto hao
 mmoja wa wajumbe ambaye jina lake alikuweza kufahamika mara moja akiwa anatandika kitanda mara baada ya kupeleka vitu mbalimbali ikiwemo shuka hizo.

  Mjumbe wa kamati ya  Jumuiya ya wazazi   ccm wilaya Arusha Phidesia Mwakitalima ambaye pia  ni mwanamke pekee ambaye alieweza kuwakilisha mkoa wa Arusha katika kinyanganyiro cha kugombea ubunge wa wazazi taifa ,akiwa anatandika shuka wakati alipotembelea mahabusu ya watoto iliopo jijini Arusha

vitanda vikiwa vinaonekana kupendeza mara baada ya kutandikwa
 katibu wa Jumuiya ya wazazi   ccm wilaya Arusha  Rehema mohamed akiwa anamkabishi afisa ustawi wa jamii mahabusu ya watoto  Mussa Mkamate selesha kwa ajili ya kukatia majani
mama akiwa anatandika kitanda




 Na Woinde Shizza,Arusha

Serekali imetakiwa kuangalia kwa makini mahabusu ya watoto ya mkoa wa Arusha kwani mahabusu hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ubovu wa majengo pamoja na ukosefu wa dawa na usafiri kwa ajili ya mahabusu hiyo.

Hayo yameelezwa juzi na baadhi ya wajumbe wakamati ya utekelezaji Jumuia ya wazazi wilaya ya Arusha wakati walipotembelea na kutoa msaada katika mahabusu hiyo ya watoto ilipo ndani ya jiji la arusha .

Kwa upande wake   katibu wa Jumuiya ya wazazi   ccm wilaya Arusha  Rehema mohamed aliitaka serekali kuangalia kwa makini sana mahabusu hiyo kwani watoto wanaoishi katika mahabusu hiyo wamekuwa wanateseka sana kutokana na mazingira ya mahabusu hiyo.

Aidha aliitaka pia mahakama kujitaidi kusikiliza kesi za watoto hao kwani wengi wao wamekaa kwa kipindi cha mda mrefu bila kesi zao kusikilizwa na badala yake wamekuwa wakiambiwa kila siku upelelezi auja kamilika.

Kwa upande wake   Mjumbe wa kamati ya  Jumuiya ya wazazi   ccm wilaya Arusha Phidesia Mwakitalima ambaye pia  ni mwanamke pekee ambaye alieweza kuwakilisha mkoa wa Arusha katika kinyanganyiro cha kugombea ubunge wa wazazi taifa alisema kuwa serekali inatakiwa   kuangalia kwa makini sana mahabusu  ya  watoto kwani mbali na hivi pia mahabusu hii watoto wakiumwa wanapelekwa hospital na pikipiki hakuna gari ya mahabusu saa nyingine dawa zinakosekana na maafisa kujikuta wakijipapasa mifukoni mwao kunusuru watoto umauti usiwakute. 

Alisema kuwa wao kama wazazi wamekuwa wanaumia sana kuona watoto hawa wakiteseka kwani  watoto hawa wanayo haki kama vile watoto walioko nyumbani uku akiomba halmashauri ya jiji la Arusha kuwakumbuka watoto hawa ata kwa vyakula na matunda .

"kuna haya matunda ambayo halmashauri ya jiji wakuwa wanayakamata kwa wafanya biashara ambao wanauza bidhaa zao sehemu ambazo si staili sasa napenda nitoe wito kwa mkurugenzi pamoja hata na mkuu wa mkoa iwapo wanakamata matunda haya na vyakula hivi wawaletee watoto hawa ili nao wakiwa uku ndani wakila wajisikie nao kama watoto waliopo majumbani "alisema phidesia

Aidha alitumia nafasi hiyo kuiomba serekali iwasaidie kuwaletea watoto hawa walimu ambao wataweza kuwafundisha masomo mbalimbali ata yakiwemo ya veta ili pale ambapo kesi zao zitasikilizwa na hukumu kutolewa huku wengine wakiwa wamemaliza hukumu zao waweze kutoka na ujuzi ambao utawasaidia pale ambapo wataenda uraiani.

"unajua wakipata elimu kuanzia huku ata akiedea mtaani ataweza kushirikisha na makundi mabovu au naweza kusema mabaya ambayo anaweza kukaanayo na kumfanya afanye uhalifu na badala yake  mfano amejifunza ujenzi akienda kule anaendelea kutengeneza vitu vyake   vitakavyomuingizia kipato"alisema Phidesia

kwa upande wake Afisa ustawi wa jamii mahabusu ya watoto Arusha  Mussa Mkamate alisema kuwa wanashukuru kwa msaada huo ambao wamepelekewa kwani utawasaidia kwa kiasi kikubwa huku akiwasihi wadau wengine kujitolea kwenda kutembelea watoto hao na mahabusu hiyo.

Aidha alisema kuwa mahabusu hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ambapo alisema kuwa mbali na ambazo zimetajwa pia wanatatizo kubwa la choo cha kutumia mahabusu hao kwani ,mahabusu hao wamekuwa wakitumia choo kimoja na uku akitolea mfano wa mahabusu ya watoto wa kiume wapo 48 lakini wanatumia choo kimoja .


Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post