Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa anaongea na wananchi wa kata ya Mang'ola hiii leo wakati alipofanya ziara katika kata hiyo iliopo ndani ya wilaya ya karatu mkoani Arusha
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa anajaza mchanga kwa ajili ya kufetua matofali hiii ikiwa nimoja ya mradi ambao ameutembelea katika kata hiyo
diwani wakata ya mang'ola Lazaro Gege akiwa anampa maelezo kwa ufupi ya mradi wa matofali kaimu katibu mkuu wa vijana CCM taifa
Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa ccm Mkoa Arusha Sabaya Lengai akiwa anaongea na wananchi wa kata ya Mang'ola hii leo wakati wa ziara ya kaimu katibu mkuu wa vijana taifa |
baadhi ya wananchi wakiwa wanaendelea kufatilia mkutano huo
Na
Woinde Shizza,Karatu
Wananchi
wa kijiji cha Malekichanda kilichopo katika kata ya Mang’ola wilayani karatu mkoani Arusha wamelalamikia
kitendo cha serekali kufungia ziwa Eyasi na
kusema kuwa kitendo hicho kimewafanya vijana wengi kukosa kazi na
kinaweza kusababisha wananchi wa eneo hilo kukubwa na baa la njaa kutokana na
kumaliza chakula chote ambacho walikuwa
wamekiifazi kwa ajili ya chakula cha akiba akiba.
Hayo
waliyasema leo wakati Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka alipofanya ziara yakutembela na kukagua baadhi ya
miradi inayofanywa na chama pamoja na
kuongea na wananchi wa kata hiyo.
Walisema kuwa
wanasikitishwa sana na kitendo cha mkuu
wa wawilaya kuwasimamisha shughuli zao za uvuvi kwani ndizo walizokuwa
wakizitegemea katika kujipatia kipato
pamoja na chakula katika kijiji hicho na kata kwa ujumla.
Mmoja wa wananchi
hao aliyejitambulisha kwa jina Kristopher Nyato alisema kuwa tangu marchi 19
walizuiwakufanya shughuli zao za uvuvi katika eneo hilo na kupewa masaa 24
kuondoka katika eneo hilo kwakile kilichodaiwa kuwa eneo hilo limekubwa na
ugonjwa wa kipindu pindu.
“unajua mimi
ni mfanya biashara nimetokea mbali nasio mimi tu tupo wengi naninavijana
wangu ambao nimekuja nao hapa kwa ajili ya shughuli hii ya uvuvi sasa tarehe hiyo
19 mwezi wa tatu mkuu wawilaya alikuja apa na askari nakutupa masaa 24
tuwe tumeondoka kuhoji nini ni wakatuambia
ni pachafu mara waseme kuna
kipindu pindu tukawaambia kama ni pachafu watuache wakagoma wakasema tumesema
muondoke ndiposisi kwa kuwa tunaogopa
nakamaunavyojua wananchi tulivyo waoga tukaondoka na tulivyoondoka
walituambia baada ya siku chache wangefungua
lakini adi sasa apajafunguliwa
tunateseka sana ata vyakula vyetu vya akiba tumemaliza yaani apa ni tabu
tu”alisema Nyato
Kwa upande wa
mwananchi mwingine aliejitambulisha kwa jina la Wiliam Jonas alisema kuwa mara
baada ya ziwa hilo kufungwa wamekuwa wanaishi maisha ya kuomba omba ,wao kama
wananchi wanagawana chakula walichokuwa wamekiifadhi na kinakaribia kwisha na
vijana wengi walikuwa wakifanya shughuli za uvuvi katika ziwa hilo wamekuwa
wazururaji.
Akiongea na
wananchi hao Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka alisema kuwa
yeye kama katibu amesikia malalamiko yao naatayafanyia kazi kwa kukutana
na mkuu wawilaya nakuona ni jinsi gani ambavyo wataweza kutatua tatizo hilo.
Gazeti hili
halikuishia hapo ilibidi kumtafuta mkuu wa wilaya ya karatu Omary Kwaanq ili kuzungumzia tuhuma hizi nakusema kuwa kweli wamelifunga
ziwa hilo kutokana na ugonjwa wa kipindu pindu ambao umeikumba wilaya yake .
Alisema kuwa
mpaka sasa wilaya yake ina wagonjwa 70 wa kipindu pindu na wamefanya utafiti
ukaonyesha wagonjwa wengi wametokea maeneo ya ziwa hilo.
“tumefanya
utafiti kiukweli kwa kushirikina na mtaalamu wamagonjwa wa milipuko nakubaini
kuwa maji yale ya ziwa yana chembe chembe za wadudu wanao eneza ugonjwa wa
kipindu pindu hivyo tukaamua ni borakufunga ziwa ilo ili wananchi wasiendelee
kuzurika na ugonjwa huo.
Aliongeza kuwa
mara baada ya kuona maji yale ya ule mto yana vimelea vya ugonjwa wa kipindu
pindu ndio maana wakaona ni bora wafunge ziwalile ili wananchi wasiendele kupata ugonjwa huo
hatari.