Na Woinde Shizza,Arusha
Serekali imetakiwa kuboresha mazingira yakuwezesha biashara ili kuweza kuongeza uwekezaji wa sekta binafsi kwenye sekta ya kilimo .
kufanya hivyo kutasaidia kupunguza tatizo la ajira ambalo ndio kero kubwa inayosumbua vijana wengi hapa nchini kwani sekta hii ya kilimo kupitia kilimo cha mboga mboga matunda na mauwa (horticuture) kinawezesha vijana wengi kujiajiri na kutoa ajira kwa vijana wengine.
Haya yalibainishwa jana na naibu afisa mtendaji mkuu (maendeleo) wa asasi kilele ya kilimo horticuture (TAHA) Anthony Chamanga wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo alisema kuwa iwapo kilimo hichi kitatiliwa mkazo basi kitamnufaisha mwananchi pamoja na nchi kwa ujumla kwa kumpatia kipato.
Alisema kuwa iwapo serekali itasaidia kuboresha mazingira ya kuwazesha biashara itasiadia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la ajira pamoja na kuongeza patao la taifa kwani wakulima watalima na mazao yatakayo patikana yatauzwa na kuwasaidia kuingiza kipato cha mkulima pamoja na kuongezea pato la taif a kwani mkulima atalipa kodi na kuileta nchi faida kwa ujumla.
Aidha pia aliiomba serekali kusaidia sekta hii kwa kuboreshas miundo mbinu ya umwagiliaji pamoja na upatikanaji wa masoko katika sekta ya horticuture.
Alibainisha kuwa ukimwezesha mkulima wa horticuture kulima kilimo cha kisasa na kitaalamu hii itamuezesha mkulima kuweza kuifadhi mazao yake baada ya kuvuna ili aweze kupata bei nzuri sokoni na pia itamuezesha mkulima kuweza kupata mnunuzi mapema na moja kwa moja bila ya kupitia kwa madalali.
Alisema kuwa mbali na changamoto hiyo pia kunachangamoto kubwa ya mabadiliko ya hali ya hewa kwani kilimo hicho kinaitaji maji mengi na kilimo hicho akiwezi kufanyika sehemu ambayo aina maji hivyo ni muhimu wakulima kufaata sheria kanuni na kununua mbegu bora ambazo zinaeza kutunza mazingira na ambazo zitahakikisha matumizi sahii ya maji.
“navyosema kutunza mazingira na matumizi sahii ya maji ni kwamba wakulima wanapaswa watumie mbinu bora zitazotunza mazingira na ambazo zinatunza matumizi ya maji na h ivyo tunapaswa tutumie teknolojia ya kutumia maji kwa kuifadhi mfano tunaweza kutumia umwagiliaji wa matone ili kuweza kutunza maji na kutumia maji kidogo au pia tunaweza kuifadhi maji kwa kutengeneza bwawa ambalo linaplastiki ndani na sisi wakulima pia tunajua kunasheria ya matumizi ya maji hivyo ni muhimu kila mkulima kufuata sheria ya maji na kupata kibali kabla ya kuanza kutumia au kuifadhi maji hayo”alisema Chamanga
Chamanga aliitaka serekali ipitie tena sera ya kilimo kwani baadhi ya vifungu vilivyopo katika sera hiyo avijakaa vyema na vingine avijajitosheleza kikanuni na vinapelekea kuwaumiza wakulima wa horticulture.
Alisema kuwa upatikanaji wa pembejeo umekuwa mgumu sana haswa kwa upande wa pembejeo za kisasa pamoja naupatikanaji wa madawa ya mimea imekuwa mgumu kutokana na baadhi ya sera hizo hivyo aliisihi serekali kupita tena sera hizi na kuzirekebisha ili kumuezesha mkulima kufanya kilimo cha kisasa na chenye tija kitakachomnufaisha mkulima pamoja na serekali kwa kuongeza kipato.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia