Ticker

6/recent/ticker-posts

UVCCM ARUMERU WALAANI KITENDO CHA MWENYEKITI WA MKOA KUMSIMAMISHA KAMANDA WAO



  Akizungumza na waandishi mara baada ya baraza hilo kukutana
jana,Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Arumeru, Boniface Mungaya
baadhi  ya  wajumbe waliouzuria mkutano huo
  Na Woinde Shizza,Arusha
BARAZA la Umoja  wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi  (UVCCM) wilaya ya
Arumeru umelaani kitendo cha UVCCM mkoani hapa kumsimamisha kamanda wa
umoja wa Vijana wa UVCCM wilaya ya Arumeru Mathias Manga kutokana na
kuisaliti CCM  katika uchaguzi mkuu wa mwa Oktaba 25 mwaka jana.
  Aida baraza hilo limelaani tamko lililotolewa wiki iliyopita na
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha,  Lengai  Sabaya na kumtaka ajitathmini
na kujipima kama anafaa kuendelea kuwa mwenyekiti wa mkoa,kama ataona
hawezi ajing'oe mwenyewe.
  Akizungumza na waandishi mara baada ya baraza hilo kukutana
jana,Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Arumeru, Boniface Mungaya,aliesema kuwa
wanamtambua  Manga ambaye pia ni  mjumbe wa Halmashauri kuu ya taifa
(NEC),kama Kamanda wao wa vijana.
  "Tunalaani tamko lililotolewa na Mkoa na hatumtambui kamanda
mwingine,Kamanda wetu hajatendewa haki,wajumbe wa baraza la tumetathmini
tamko la Lengai tunaona ni ukiukwaji mkubwa wa kanuni,amepoka madaraka
yasiyo yake,kitendo ambacho ni kurudisha chama nyuma badala ya
kukijenga"alisema na kuongeza
  "Sabaya ajitathmini,ajipime kama anafaa kuendelea kuwa mwenyekiti wa mkoa
kwani tunaona akiendelea hivi kukiuka kanuni atakiua chama,ni bora ajing'oe
mwenyewe kama anaona hawezi,tunampa siku saba akanushe madai aliyoyatoa
dhidi ya kamanda wetu"
  Alisema kuwa tamko hilo ni batili na hawalitambui na  kumtaka Manga
asivunjike moyo aendelee na haratkati za kukijenga chama hivyo asirudishwe
nyuma na changamoto anazokabiliana nazo.
  Akizungumzia yeye kuwepo kwenye baraza hilo alidai kuwa siku ya kikao
alikuwepo ila alikataa kupiga kura ya kumkataa Kamanda wake na kuamua
kutoka nje.
  Naye Anjelina Lukumay ambaye ni mjumbe wa baraza hilo kutoka Kata ya
Oldonyosambu,alimuomba Mwenyekiti wa CCM mkoani hapa,Lekule Laizer
kuliangalia suala hilo na kulitafutia ufumbuzi kwani Sabaya amekiuka kanuni
za chama.
  "Mwenyekiti wa wilaya ametumia kanuni ipi kumkataa kamanda wetu bila
kutushirikisha?hatutakubali kuvurugwa wilaya ya Arumeru,tumepokea kwa
mfadhaiko kauli hiyo kwani Sabaya kachaguliwa hata miezi miwili hana ila
inakuwaje anataka kumtoa Manga tena bila kutushirikisha?alihoji Anjelina
  Wiki iliyopita uamuzi wa kumsimamisha Manga ulifikiwa katika  kikao cha
baraza la UVCCM mkoa wa Arusha kilichozinduliwa na kaimu katibu mkuu Shaka
Hamdu Shaka,ambapo kikao hicho kilikuwa na wajumbe 34 huku 33 kati yao
wakipiga kura za ndiyo.
  Pia kikao hicho kilitoa onyo kali kwa kamanda wa UVCCM wilaya ya Arusha
Mjini,Longido na Monduli na kuwataka wajipime na kujitathimini kama
wanatosha kuwa makamanda wa UVCCM na  wakiona hawatoshi tunaomba wakae
pembeni kabla  baraza halijawachukulia hatua.
  Uamuzi wa kumsimamisha Manga ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya
taifa (NEC)wilaya ya Arumeru   ulifikiwa katika Manga
Akisoma tamko lilitolewa na Kikao hicho cha baraza  kikao hicho cha
baraza Katibu wa Hamasa wa (UVCCM) Mkoa wa Arusha, Lucas Nsomi alisema
Manga kuanzia wakati huo  si kamanda wa Vijana Wilaya ya Arumeru tena kwani
amepoteza sifa baada ya kudhibitika kukisaliti chama kwenye uchaguzi Mkuu
wa mwaka 2015,kwani wakati wa uchaguzi huo alionekana akifanya vikao
vyakufanikisha ushindi kwa UKAWA.
  “Kikubwa alichofanikiwa Manga ni kuwagawa vijana wa Arumeru hali
inayopelekea kushindwa kuijenga jumuiya hiyo na kuanzia sasa sio kamanda wa
vijana tena wa wialaya hiyo na sipo tayari kufanya naye kazi yoyote ile
ndani ya CCM”.
  Sabaya  alidai kuwa vijana waliompitisha kuwa kamanda lilikuwa ni genge
la wahuni ambao walikuwa wakiendesha vikao vya vijana wenye njaa na kuwa
hayupo tayari kuwa Mwenyekiti wa magenge ya vijana wenye njaa na wasaliti
ndani ya CCM.

Post a Comment

0 Comments