MWENYEKITI WA MTAA AWEKWA KITI MOTO KWA KUGHUSHI MUKHTASARI


 Na Woinde Shizza,Arusha

Kamati ya nidhamu yaChama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema)
kata ya Ngarenaro jijini Arusha imemweka “kitimoto” mwenyekiti wa
mtaawa mita 200,Winstone Laiser kwa madai ya kughushi mukhtasari wa
kikao chakamati ya utendaji jambo ambalo ni kinyume na sheria za chama
hicho.
Kikao hicho ni kilekinachodaiwa kuketi mnamo Oktoba 6 mwaka jana
ambacho kilihudhuriwa na wajumbewatano huku kikiwa na ajenda ya
kujadili ajenda ya  kumtambua aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kasulu,Dahni
Makanga kwamba ni mkazi wa eneohilo .
Hatua hiyo imefuatiamara baada ya baadhi ya wajumbe wanaodaiwa
kuhudhuria kikao hicho kufikisha malalamikiayao mbele ya uongozi wa
chama hicho na kulalalmikia kitendo cha majina yaokuandikwa katika
mukhtasari huo ingawa hawakushiriki kikao hicho.
Kwa mujibu wa taarifazilizolifikia gazeti hili zimedai kwamba kamati
ya nidhamu ya kata ya Ngarenaroilimhoji Laiser juzi kwa lengo la kumpa
nafasi kujibu tuhuma za kughushimukhtasari huo .
Taarifa hizo zimedaikwamba baadhi ya wajumbe katika kikao hicho
walimbana mwenyekiti huyo kwakutaka kujua kweli wa tuhuma hizo ambapo
baadhi yao walionekana kushtushwa nataarifa kwamba mukhtasari huo
unatumika kamakielelezo katika mgogoro wa kugombea ardhi ndani ya kata
hiyo.
Hatahivyo,kwa mujibu wataarifa ndani ya kikao hicho zimedai kwamba
mwenyekiti huyo alijitetea kwambaalirubuniwa na baadhi ya watu huku
akiiangukia kamati hiyo ya nidhamu kwa lengola kuiomba msamaha.
Mmoja wa wajumbe ambaoamepinga kitendo cha jina lake kutajwandani ya
mukhtasari huo ingawahakushiriki kikao hicho,Peter Lukumay alisema
kwamba wanapinga kwa nguvu zotekitendo hicho kwa kuwa wanaweza
kuingizwa katika kesi ya jinai. Alipoulizwa Laiserkuhusu taarifa za
kuhojiwa na kamati hiyo alisema kwamba aulizwe aliyetoataarifa hizo
huku akisisitiza kwamba atachukua hatua anazozijua endapo taarifahizo
zikiandikwa gazetini.
“Wewe nenda kamuulizehuyo aliyekupa taarifa hizo lakini kama ukiandika
hizi taarifa mimi nitachukua hatuaninazozijua “alisema na kisha kukata
simu
Mwenyekiti wa Chademakata ya Ngarenaro,Steven Urasa alipohojiwa kuhusu
taarifa hizo alikirikufanyika kwa kikao hicho huku akisema kwamba
anasubiri mapendekezo ya kamatihiyokabla ya kuyawasilisha mbele ya
uongozi wa Chadema ngazi ya wilaya.
Hatahivyo,mwenyekiti waChadema wilaya ya Arusha,Dereck Magoma alikiri
uongozi wake kupokea taarifahizo na kusisitiza kwamba anasubiri
maamuzi ya kikao kilichoketi kujadili sualahilo kabla hajatangaza
hatua zilizochukuliwa.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post