mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha Lengay Ole Sabaya akiwa anatoa tamko hivi karibuni
Na Woinde Shizza,Arusha
Baraza
la vijana mkoa wa Arusha la chama cha mapinduzi
uvccm limetangaza kumvua ukamanda wa vijana wilaya ya Arumeru bw,Mathias
Manga kutokana na kukiujumu chama kwa muda mrefu hali ambayo imekuwa
ikididimiza jitihada za kurejesha imani ya chama hicho.
Bw,Manga
ambaye ni mafanyabiashara maarufu wa madini Mkoani Arusha amekuwa akituhumiwa
kwa muda mrefu kuwa namhausiano ya karibu ya aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi
ya Ukawa Edward Lowassa na kusahau kufanya majukumu ya kichama ambayo yamempa
uongozi wa Ukamanda wa vijana wilaya.
Akitoa
maelezo ya tamko hilo mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha Lengay Ole Sabaya
amemtaja Mathias Manga na washirika wake kuwa ni tatizo kubwa ndani ya chama na
kwamba kama akiendelea kuwepo ni Dhahiri kuwa anaweza kukisambaratisha chama
hicho kutokana na kugawa makundi kwa vijana wa chama hicho kutokana na fedha
zake.
Aliongeza
kuwa kutokana na kumvua ukamanda kamanda huyo UVCCM Mkoani hapa haitakuwa
tayari kushiriki kikao chochote cha kamati ya siasa ambapo Manga atashiriki
kama mjumbe katika kikao hicho.
,,Sitashiriki
kwa namna yeyote na vijana wangu kwenye kikao cha kamati ya siasa Mkoa ama
kikao kingine ambacho kitanikutanisha na Mathias Manga na nawataka wanachama wa
chama cha mapinduzi kuona kama ni halali kwa huyu aliyeitwa kamanda wa vijana
kuendelea kushikilia kadi yao,,Alisema Ole Sabaya
Akitoa
onyo kwa makamanda wilaya ya Arusha mjini,Longido na Monduli kujipima na
kujitathimini kabla ya kufikia uamuzi kama bado wanafaa kuendelea na hadhi ya
ukamanda wa wilaya ama laa,na wakijiona hawatoshi tunawashauri wakae pembeni
mapema kabla ya kutumbuliwa jipu.
Baraza
linakiomba chama cha Mapinduzi kupitia tathini ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana
wale wote walioshiriki kukihujumu chama kuanzia ngazi ya matawi,kata,wilaya na
Mkoa washughulikiwe kwa mujibu wa taratibu za kimaadili kabla ya uchaguzi wa
chama 2017 vinginevyo wakiachwa watashiriki tena kufanya uhasi dhidi ya chama
sanjari na kupandikiza mamluki.
Hata
hivyo mwenyekiti huyo ametengua uteuzi wa wajumbe watano wa baraza katika
nafasi za kuteuliwa ilidumu toka mwaka 2012 na kuunda kamati mpya chini ya
mwenyekiti Lengai Ole Sabaya huku
akiwataka viongozi wa chama hicho kumuunga
mkono Rais JohnPombe Magufuli kwa jitihada
zake za kupeperusha bendera ya chama na kufanya kazi kwa uadilifu na kubeba
kauli ya HAPA KAZI TU.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia