BREAKING NEWS

Friday, April 22, 2016

ASILIMIA 18 YA SIMU ZA KIGANJANI ZAONEKANA NI BANDIA ,HUKU ASILIMIA 79 ZIKIWA SALAMA

 

Na Woinde Shizza,Arusha

MAMLAKA ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa asilimia 79 ya simu za
kiganjani  zilizofanyiwa utafiti kwa kipindi cha desemba hadi February
mwaka huu  ziko salama na sio za bandia ,huku asilimia 18 zikionekana
zikiwa za bandia  hivyo kuwataka wananchi kutambua kuwa simu  feki zilizoko
sokoni ni chache tofauti na kipindi cha nyuma.

Pia imebainika kuwa asilimia kubwa ya nyumba zinazoungua  na umeme ni
kutokana na simu bandia ambazo betri zake au vifaa vyake hushindwa kuhimili
mionzi pindi zinapokuwa zinachajiwa  hivyo kusababisha mlipuko wa moto na
hivyo kuleta madhara .

Hayo yalisemwa na meneja uhusiano wa mamlaka ya mawasiliano  Tanzania
Innocent Mungi alipokuwa  akizungumza katika semina ya mfumo wa rajisi ya
namba za utambulisho wa simu za kiganjani iliyowashirikisha wadau na
wafanyabiashara wa jijini hapa.

Alisema kuwa kutokana na elimu ambayo wameitoa kwa wafanyabiashara wa simu
hizo ya  kuhakiki kwanza kabla ya kuwauzia wananchi   imepunguza uingizaji
wa simu feki na kwamba wamebaini kuwa asilimia 79 ni salama hazina matatizo
ya aina yeyote.

Alidai kuwa kufuatia uzimaji wa simu bandia litakalofanyika juni 16 mamlaka
hiyo imeweza kutoa elimu kwa wauzaji,watumiaji ili kuhakikisha kuwa
wanabini simu zao  kama ni salama ili kuweza kuepuka zoezi la kuzimiwa simu
zao bila yawao kujiandaa.

“wakati tumeanza kubaini zoezi la kutambua simu feki tulibaini kuwa
asilimia 30 zilikuwa bandia ila kutokana na elimu iliyotolewa hadi February
simu bandia zimepungua hadi kufikia asilimia 18 hii inaonyesha kuwa simu
feki  zilizoko sokoni ni chache mno “aliongeza

Aidha Innocent alitaja faida za kuzimiwa simu bandia kuwa ni pamoja na
kuongeza usalama mtandaoni kwa watumiaji wa simu  ,kupunguza wizi wa simu
na kupunguza matukio ya uhalifu ambayo yamekuwa yakitumika mara nyingi kwa
njia ya simu hizo  pamoja na kuzuia matumizi ya simu zisizokuwa na viwango.

 Awali mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo Ally Simba  aliwataka wananchi
kufanya zoezi la kuhakiki simu zao kwa kufuata maelekezo sahii ili waweze
kubaini simu feki kabla ya kuzimiwa simu hizo  juni 16 ,kwani wengi wa
watumiaji wa simu hawafuati malekezo ya kutambua simu bandia .

Simba aliseama kuwa ni vema wananchi wakatumia mfumo waliowekewa wa kubaini
simu zao kama ziko salama kwani ifikapo juni simu zote bandia zitazimwa na
kuwataka  wafanyabiashara nao wawe makini pindi wanaponunua mizigo yao ya
bashara  ili kuepuka hasara watakazozipata wao na pia hasara watakazopata
wanunuzi wa simu hizo .

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates