Ticker

6/recent/ticker-posts

NAPE ATAJA MAJIPU MANNE KATIKA SANAA NCHINI,AHAIDI KUYATUMBUA



Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akifunua pazia kuashiria uzinduzi wa Tamasha la kimataifa la filamu la Tanzanite mjini Arusha
Baadhi ya viongozi wa Jiji la Arusha
Mkurugenzi wa Tanzanite One ambao ndio wadhamini wakuu wa Tamasha, Ndugu Faisal Juma akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Kimataifa la Filamu la Tanzanite mjini Arusha kwenye hotel ya Mt. Meru
Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza wakati wa uzinduzi wa tamasha la Kimataifa la Filamu la Tanzanite mkoani Arusha .

 Waziri Nape aliwaambia wadau na waigizaji wa Filamu waliohudhuria uzinduzi wa Tamasha hilo kuwa hii ni moja ya hatua kubwa kwenye historia ya filamu nchini na kuahidi Wizara yake itaendelea kutoa ushirikiano mkubwa na kuhakikisha haki za wasanii hazipotei wala haziliwi na wajanja.

 Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (mwenye kaunda suti ya kijivu) akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Ndugu Felix Ntibenda  kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Arusha pamoja na wadhamini kwenye uzinduzi wa Tamasha la Kimataifa la Filamu la Tanzanite.

 Baadhi ya watu waliohudhuria uzinduzi huo wa Tamasha la Filamu la Kimataifa la Tanzanite.
Yvonne Cherry 'Monalisa' pamoja na mama yake, Suzan Lewis 'Natasha' (katikati) wakifuatilia sherehe uzinduzi wa Tamasha la Filamu la Kimataifa la Tanzanite kwenye hotel ya Mt. Meru
Waziri wa Habari,Utamaduni,sanaa na michezo nchini,Nape Nnauye
ametaja mambo manne ambayo ni vikwazo ndani ya sekta ya sanaa ya filamu
nchini na kuyaita kwamba ni majipu huku akisisistiza kwamba serikali
itakwenda kutunga sera ya sekta hiyo katika mwaka wa fedha 2016/17.

Nape,aliyataja mambo hayo na kuyafananisha na majipu kuwa ni uporaji wa
kazi za wasanii nchini,ujenzi duni wa miundombinu ya kazi za wasanii
nchini,usimamizi mbovu wa bodi ya filamu nchini sanjari na tatizo la mfumo
mbovu wa usambazaji wa kazi za wasanii nchini.

  Akizindua tamasha la filamu la Tanzanite International Film
Festival(TIFF) jijini Arusha juzi ambao ulihudhuriwa na wasanii maarufu wa
filamu nchini waziri huyo alisema kwamba jipu la kwanza ambalo atakwenda
kulitumbua ni uporaji wa kazi za wasanii nchini.

  “Jipu la kwanza tutalitumbua kwenye bajeti yetu ya mwaka 2016/17 ni
uporaji wa kazi za wasanii nchini wengi wananyonywa jasho lao”alisema Nape

  Hatahivyo,alisema kwamba jipu la pili ni ujenzi duni wa miundombinu ya
kazi za wasanii za filamu nchini na kudai kwamba chini ya uongozi wake
atahakikisha anaimarisha miundombinu bora kwa lengo la kuwasaidia wasanii
hao pamoja na kulinda haki zao.

  Alisema ya kwamba mfumo wa kazi za usambazaji wa kazi za wasanii nchini
pamoja na hakimiliki ni wa kinyonyaji huku akitolea mfano wa kazi za msanii
maarufu wa sanaa hiyo nchini marehemu Stephen Kanumba na kusema kwamba
familia yake hainufaiki na matunda ya kazi zake hadi sasa kutokana na mfumo
mbovu wa usimamizi wa kazi za wasanii nchini.

  Alitaja takwimu kwamba mwaka 2011/12  jumla ya filamu 218 zilitengenezwa
nchini na mwaka 2014/15 kazi hizo ziliongezeka hadi kufikia 14,00 huku
akidai hilo linadhihirisha kwamba sekta hiyo inakua kwa kasi nchini na
kuongeza ajira .

  Hatahivyo,Rais wa shirikisho la wasanii wa filamu  nchini(TAFF),Simon
Mwakifamba aliwataka wasanii wa filamu nchini kujiandaa kisaikolojia
kukabiliana na soko la ushindani wa filamu duniani kwa kuwa wabunifu.

  “Serikali tunaiomba iandae sera itakayoandaa mazingira mazuri kwa wasanii
nchini kuhusu usalama wa kazi zao”alisema Mwakifamba
Naye, muaandaji wa tamasha hilo,Said Sassi alisema kwamba tatizo la
uharamia wa  kazi za wasanii nchini  limetanda na kuwaomba wafanyabiashara
na makampuni kujitokeza kudhamini vipindi mbalimbali vya luninga kwa lengo
la kuinua sekta hiyo.

  Mkurugenzi wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya vito ya Tanzanite One
Mining Ltd ambao ni  miongoni mwa wafadhili wa tamasha hilo,Feisal Shabhai
alisema lengo la kampuni yao kujitosa kufadhili tamasha hilo ni kutoa
mchango wao katika kusaidia jamii kupitia faida wanayoipata ili kuinua
sekta ya ajira nchini.

Post a Comment

0 Comments