Na Mwandishi Wetu ,Zanzibar
Wakati kukiwa taarifa hali ya ustawi wa kisiasa si shwari ndani ya CUF watoto wawili wa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Mji Mkongwe kwa chama hicho Ibrahim Sanya wamejitoana kuamua kujiunga na CCM kupitia UVCCM.
Wahid na Jamal Ibrahim Sanya wakiisema kwa nyakati tofauti wakielezea jinsi waluvyochoshwa na siasa za cuf chini ya uongozi wa Katibu Mkuu wake Maalim Seif Sharif Hamad na sasa wamehamaia rasmi ccm.
Katika mkutano wa uzinduzi ulioitishwa na kundi la kiharakati la vijana wanaaojulikana kwa jinanla G ONE uliofanyika juzk huko Maruhubi nje kidogo ya mji wa Unguja , Jamal alisema baada ya kutafakari, kujipima na kujiridhisha hatimaye akapata jawabu sahihi lililomfamya ayosheke kukiuga mkono cuf na kukihama chama hicho.
"Akili kama mjjuavvyo ni jambo la ajabu katika mumble ya binadamu, akili zile zile zilizonishawishi miaka ile niiunge cuf ,ndo akili hizi hizi sasa zinanielekeza nijitoe chama hicho na kuhamia ccm" alisema Jamal.
Kwa upande wa ndugu yake Wahid , alisema pamoja na kipndi kirefu baba yake kuwa mbunge wa jimbo la Malindi baadae kikabadilishwa na kuitwa Mji Mkongwe, fikra zake zimemuelekeza ajiondoe cuf na kujiunga ccm bila kushswishiwa au kuruhusiwa.
"Nimehama cuf leo mimi na ndugu yangu kwa hiari yetu, tunechoshwa na siasa zenye mizengwe na upendeleo .2ni siasa dhaifu na mbaya ndani chama hicho, sasa tunafikiria kumshauri baba yetu akikubali akihamie ccm "alieleza Wahid
Baba wa watoto hao anbaye ni mwanasiasa maarufu katika siasa za zanzibar Mohamed Sanya alishika ubunge kupitia CUF tokea mwaka 1995 hadi lakini aliposhiriki kura za maoni ndani ya cuf mwaka jana aliweza kushima nafasi ya kwanza ongoza ila aktima hali ambayo haikutazamiwa jina lake kikikatwa na kuteuliwa mshindi wa tatu ambaye sasa ni mbunge wa jimbo la Mji Mkongwe Mwanasheria Ali Saleh
Habari za uhakika toka ndani ya cuf jimbo la Mji Mkongwe zinahabarisha kuwa Sanya licha ya kuongoza kura za maoni jina lake kikikatwa kwa madai alitoa maneno ya kibri dhidi ya Maslim seif.
Kiongizi mmoja machachari katika tawi la Mkunazini mjini Unguja , akieleza na kuasa jina lake lisiandikwe gazetini.
Akisema Maalim seif aliwahi kusikia akishauri ni wakati muafaka kwa sanya akapumzika na kuwaachia wengine baada ya kushika ubunge miaka 20.
"Maneno hayo yalimkera sanya hivyo kupitia watu wale wale sanya akasema hata naye anafikir Maalim seif asiwania urais wa zanzkbarbadala yame amqavhie Hamad Rashid Mohamed au Mohamed Abdulrahman Dedes.
"Kama mimi nimewania vioindi vinne maakim seif anewani mara suta rikea mfumo wa vhama kimoja na mara tamo kwa gyama bingi"alinukukiwa sanya akisema.
Aidha Mtoa taarufa wetu akaeleza kuwa majibu hayo ya sanya yakimchukiza mno Maalim seif na kuahidi angemshughuiikia sanya kamaba ambavyi Hamad Rashid alivyotupwa nje ya chama hivho.
Katka kile linachoelezw ni mkakayk wa kummaliza sanya kisiasa , , jina la mgombea huyo likikatwa chini ya ukatibu mkuu wa Maalim seif kwenye kikao cha Baraza kuu la cuf .
Raia Tanzani licha ya kuchukua juhudi za kumtafuta Mkurugenzi wa miipango na uchaguzi wa cuf Omar Ali Shehe au mbunge wao wa zamanj Sanya, simu zao mara zote ziliita bila kupokewa.
Tokea jina la sanya kukatwa kumekuwa na mbwembwe nyingi zilizokuwa zikifanya mfukulizo na wafuasi wa Ali Saleh kama vile kuchinja mbuzi, kunywa kahawa kwa halua huku mashabiki hao wakimshambulia huku wakihanikiza maneno ya kejeli dhidi ya sanya nje ya nyumba yake