BREAKING NEWS

Thursday, April 14, 2016

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA ARUSHA AWATAADHARISHA WANACHAMA WASIONA MSIMAMO KUWA NI JIPU NA WAJIENGUE WENYEWE KABLA AJAWATUMBUA

 Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha Lekule Laizer akiwa anaongea na wananchi wa tawi la chama cha mapinduzi Simba lililopo ndani ya kata ya Mbulumbulu
 Katibu wa itikadi na uenezi wa mkoa wa Arusha Shabani Mdoe akiwa anaongea na wananchi wa kata ya mbulumbulu wakati wa ziara ya viongozi wa mkoa wa chama cha mapinduzi



 Katibu wa itikadi na uenezi wa mkoa wa Arusha Shabani Mdoe akiwa anaongea na wananchi wa kata ya mbulumbulu wakati wa ziara ya viongozi wa mkoa wa chama cha mapinduzi

 Katibu  wa ccm wialaya ya karatu Loth Olelemeiruti akiwa anaongea na wananchi
 mmoja wa wananchi wa kata ya mbulumbulu akiwa anamueleza mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha matatizo  yanayowakabili katika kata yao ikiwemo  ukosefu wa barabara


 Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha Lekule Laizer akiwa na baadhi ya viongozi wa matawi wa ccm wa kata ya mbulumbulu  wilayani karatu mkoani Arusha

Na  Woinde Shizza,Karatu

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha Lekule  Laizer amewaagiza viongozi wa  matawi  wa kata ya mbulumbulu na wilaya ya karatu kwa ujumla  kufanya tadhimini ya uchaguzi uliopita haraka iwezekanavyo na kupeleka majibu  kwa katibu wa chama cha hicho wilaya ya karatu  Loth Olelemeiruti  ili kuweza kujua ni watu gani ambao waliweza kuhujumu chama na kuchukuliwa hatua kali.



Hayo aliyasema jana  wakati alipokuwa akiongea na wanachama wa chama cha mapinduzi  ndani ya kijiji  cha Losteti  kilichopo ndani ya kata ya mbulumbulu wilayani Karatu Mkoani Arusha  .



Alisema kuwa katika uchaguziwa uliopita baadhi ya viongozi pamoja na wananchama waliweza kusaliti chama kwa kutoa siri za chama pamoja na kuwapa ushirikiano viongozi wa upinzani hali ambayo ilichangia kwa kiasi kikubwa kupoteza baadhi ya kata.



“napenda kuwaambia viongozi wote wa matawi wafanye tadhimini haraka iwezekanavyo baada ya hapo wapeleke majibu kwa katibu wa wilaya ya karatu ili aweze kuyafikisha mkoani na sisi tuweze kuyatumbua majipu yote ambayo   walikisaliti chama wakati wa kampeni”alisema Laizer



Aidha aliongeza kuwa sasa ivi viongozi wa chama wanatakiwa kufanya kazi kama kwa nguvu zao zote pamoja na akili zao zote ili kuhakikisha chama kinarudi katika mstaari wake na sio hivyo tu iwapo viongozi watafanya kazi kwa nguvu zao zote itasaidia pia kumpa nguvu rais wa nchi ambaye ametoka katika chama cha mapinduzi.



“tunajua watu wengi walichukuliwa na mafuriko sasa napenda kusema yale mafuriko yameisha sasaivi ni kazi tu ,na pia napenda kutumia fursa hii kuwaambia wananchi yeyote ambaye anataka kuwa mwana chama wa ccm achukuwe kadi mapema kwani itafikia mahali chama akitatoa kadi tena na sio kuchukuwa kadi tu bali kulipia ada maaana mwanachama ambaye ajalipa ada ya uanachama basi yeye sio mwananchama hai kwakua ajalipa ada ni bei ndogo sana kwa iyo kila mwanachama anatakiwa alipe ada ili awe mwanachama hai”alisema Laizer

Alibainisha kuwa kwa sasa amana kiongozi ambaye atachaguliwa kwa kutegemea rushwa hivyo ,kama kunamwananchi au mwanachama ambaye anategemea aje achukuwe fomu katika chaguzi zijazo kwa kutoa rushwa au anategemea atatumia pesa zake kushinda katika uchaguzi asahau kabisa maana sasa ivi ndani ya ccm awataki watu ambao wanatumia fedha kupat a nafasi za uongozi  wamepotea kwani aita kubalika kabisa.

Hata  hivyo mwenyekiti huyo amejinasibu kuwa aliyekuwa mgombea wa urais kupitia umoja wa vyama vinavyounda ukawa  Edwad lowasa kamwe atakaa aje kuwa rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kulingana na mazambi yake  aliyoyafanya  kwani amefanya nae kazi kwa muda mrefu na anafahamu vizuri.

Kw aupande wake katibu wa itikadi na uenezi mkoa wa Arusha Shabani Mdoe amesema kuwa wao kama viongozi wa chama wamejitoa sadaka kwa ajili ya kuimarisha chama cha mapinduzi  mkoa wa Arusha na watafanya kila jitiada kuhakikisha chama kina simama imara na iwapo kunamtu ndani ya chama anaejijua kuwa ni jipu aanze kujitumbua mapema kabla ajatumbuliwa .

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates