*Timu ya soka ya polisi ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani
Manyara, imeifunga mabao 5-0 timu ya Mirerani Veterani kwenye mchezo wa
kirafiki uliofanyikwa katika uwanja wa barafu. *
*Wachezaji wa polisi wakiongozwa na kocha wao, mkuu wa kituo cha polisi
Mirerani (ASP) Thomas Mniko, walitawala pambano hilo kwa muda mrefu kwenye
vipindi vyote viwili vya mchezo huo ulifanyika juzi.*
*Mabao ya timu ya polisi yalifungwa na mshambuliaji wao hatari Julius Mdaki
aliyefunga magoli matatu kwenye dakika ya 30, 40 na 60 huku winga wao
Emmanuel Makasi akifunga magoli mawili katika dakika ya 70 na 80. *
*Nyota wa mchezo huo, golikipa wa timu ya polisi Charles Mabanda
alifanikiwa kuokoa michomo mikali ikiwemo penati ya timu ya Mirerani
iliyopigwa na Ally Ajemy huku penati ya mchezaji mwingine Mwalimu Hamis
ikiota mbawa.*
*Hata hivyo, timu ya Mirerani Veterani ikiongozwa na hakimu wa mahakama ya
Godfrey Haule, japokuwa ilifungwa mabao 5-0 nayo ilitoa burudani ya kutosha
kwa mamia ya washabiki waliojitokeza kwa wingi kuangalia mchezo huo. *

Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia