picha maktaba ya madereva toyo
Na Woinde Shizza,Arusha
Waendesha bodaboda wametakiwa kukwenda kwenda darasana
kupata elimu ya usalama barabarani ili kuweza kuepusha ajira za maramara kwa
mara zisizo tarajiwa .
Haya yalibainishwa na diwani wa viti maalumu kupitia chama
cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kata ya Usariver Mary Antony wakati akiongea na madeva bodaboda hao mara
baada ya kuwalipia ada ya mafunzo ya
usalama barabarani madereva 45 wa kata ya usa river.
Alisema kuwa ni wajibu wa kila dereva bodaboda kwenda kupata
elimu ya usalama barabarani ili kuweza kupunguza ajali za barabarani
zinazotokea mara kwa mara kwa kusababishwa na uzembe wa madereva hao.
“mimi kama diwani wa viti maalumu niliamua kwenda kuwapatia
kuwalipia ada ya mafunzo madereva hawa
wa bodaboda ili angalau waweze kujua sheria za barabarani na pia waweze kupata
leseni maana hawa wote awana lesini na sio ivyo tu nadhani iwapo madereva hawa
watazijua izi sheria za bara barani hii itasaidia kupunguza ajali za mara kwa
mara ambazo zinatokea”alisema Mary
Alibainisha kuwa ni wajibu wa kila dereva kujua sheria na
iwapo atajua sheria watajiamini na pia
awatasumbuliwa ata na polisi wa usalama
barabarani njiani kwani watakuwa wanajua sheria hivyo ata akiambiwa amefanya
kosa ataweza kujua ni kosa kweli au amedanganywa kwakuwa tayari anajua sheria
hizi za usalama wa barabarani.
Kwa upande wake mmoja wa vijana wa bodaboda wa kata hiyo ya
Usariver alisema kuwa anamshukuru diwani huyo kwa kuwasaidia kwani
wamejitambua na wajua sheria na
aliwasihi madereva wenzake kwenda mashuleni kujua sheria hizo.
Alisema kuwa mafunzo hayo ambayo wameyapata yatawasaida
kujiamini na pia yamewasaidia pia
kutowaogopa askari wa barabarani kama
zamani kwani kwa sasa wanajua sheria ya usalama barabarani na sio hivyo tu
katika mafunzo hayo pia wamefundishwa mafunzo ya ulinzi shirikishi ili
kuwezakuwatambua wezi na jinsi ya
kujiepusha na wateja ambao hawawaeliwi kwani kipindi hichi madereva wengi
wanaibiwa pikipiki zao.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia