Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Waziri wa Kilimo, Maliasil, Mifugo na Uvuvi Hamad Rashid Mohamed amekutana na wakulima wa kilimo cha mwani kwa lengo la kusikiliza na kubaini sababu ya kushuka bei ya zao hilo viswani humu.
Hamad aliwatembekea wavuvi hao katika Wilaya ya Kati Mmkoa wa Kusoni Unguja ili kusikiliza malalamiko ya wakulima kufuatia kushuka bei ya zao hilo toka shilingi 600/700 hadi 400/300 .
Mwani ni la pili kwa wingi na la tatu katika kuchangia pato la Taifa visiwani humu.
Takriban wakulima wanaofikiri 23, 500 sawa na asilimia 90% wengi wakiwa wanawake , huzalisha wastani wa tani 16500 kila mwaka visiwani zanzibar .
Waziri Hamad, aliwaahidi wa kulima hao kuwa ifikapo jumatano serikali ya Mapinduzi Zanzbar itatatangaza kiwango cha bei elekezi ya zao la mwani.
Alisema pia smz itaeleza jinsi ya ushiriki wa shirika ZSTC katika ununuzi wa mwani pale ambapo sekta binafsi inaposhindwa kununua au kupanga bei isio na tija wala faida kwa wakulima.
"Nitazungumza na wawekezaji kwa lengo la kuanzisha viwanda vya kuusarifu mwani wenye matumizi zaidi ya nane( 8 ) , upo uwezekano wa kuongeza thamani, serikali atajitahidi kuangalia uwezekano wa kupumguza gharama za uzalishaji " alisema Hamad
Hata hivyo mara baada ya maelezo hayo toka kwa Waziri huyo dhamana wakulima wa zao hilo walionyesha kufurahia msimamo wa serikali na kujengeka matumaini mapya chini ya Wizara kilimo, mifugo, maliasili na uvuvi.
Wakulima walielezea matumaini yao wakisema ni fahari kuona Waziri mhusika wa Serikaii akiwa kiongozi wa kwanza kutembelea maeneo ya bahari ambako wakulima wa zao hilo hufanya ukulima na uzalishaji.