BREAKING NEWS

Friday, April 8, 2016

VITUO VYA POLISI VYAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA UCHAKAVU


Na  Woinde Shizza,Arusha.
Vituo vingi vya polisi hasa vile vilivyopo pembezoni mwa miji vimekua vikikabiliwa na changamoto ya uchakavu wa majengo,uhaba wa majengo pamoja na vitendea kazi suala ambalo linapunguza kasi ya jeshi la polisi katika kupambana na uhalifu.
Hayo yameelezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha aliyemaliza muda wake Liberatus Sabas amesema kuwa uhaba wa majengo na vituo katika maeneo ya vijiji umekua ukipunguza ufanisi wa kazi ya polisi katika kulinda raia na mali zao hivyo ameitaka serikali kukarabati vituo hivyo pamoja na kuweka vitendea kazi vya kutosha.
Akizungumza katika uzinduzi wa kituo kipya cha polisi cha Tengeru kilichozinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda amesema kuwa hatua ya kuboresha vituo vya polisi itasaidia kutatua kero za kiusalama zinazokabili maeneo mengi mkoani Arusha.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meru amelitaka jeshi la polisi kuwachukulia hatua baadhi ya polisi ambao huwabambikia wananchi na kujihusisha na vitendo vya rushwa ambavyo huwaumiza wananchi wengi
Mkuu wa Mkoa wa Arusha aliyezindua kituo hicho amewataka Wananchi wa kushirikiana vyema na jeshi la polisi katika kutoa taarifa za uhalifu ili kutokomeza vitendo vya uhalifu vinavyojitokeza kila mara

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates