MIGOGORO ya ‘mitoboano’ katika migodi ya
Tanzanite, imechukua sura mpya, baada ya mlinzi wa mgodi wa Joseph
Mollel, maarufu kama Papa King kupigwa risasi.
Akizungumza
katika wodi ya majeruhi ya Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru,
mlinzi wa mgodi huo, Joseph Thomas (20), alisema alipigwa risasi na
mmiliki wa mgodi jirani.
Alisema akiwa chini ya mgodi huo Jumanne wiki hii, wachimbaji wa mgodi jirani walitoboa hadi kwenye mgodi wao na kujaza udogo.
Alisema baada ya kutoka nje ya mgodi ugomvi kati yao ulizuka na
ulipozidi mmliki wa mgodi huo (jina limehifadhiwa), aliingilia kati na
baadaye akampiga risasi.
Alidai kuwa alilengwa kichwani, lakini alipokwepa bahati nzuri risasi hiyo ilimpata mguuni.
Alisema tukio hilo lilitokea saa 7 mchana na baada ya meneja wa mgodi huo kutoa taarifa polisi, alifikishwa hospitalini saa 6: 00 usiku.
Alisema tukio hilo lilitokea saa 7 mchana na baada ya meneja wa mgodi huo kutoa taarifa polisi, alifikishwa hospitalini saa 6: 00 usiku.
Akizungumzia tukio hilo, Meneja wa mgodi huo, Elikana Sanayo, maarufu
kama Nyundoo, alisema baada ya tukio hilo alitoa taarifa polisi na
ofisi ya madini na kumpeleka hospitali kwa matibabu.
Daktari aliyempokea, Abraham Maro, alithibitisha jeraha alilopata mlinzi huyo lilitokana na risasi.
Alisema baada ya uchunguzi wa kitabibu tuligundua jeraha hilo lilitokana na risasi.
Alisema baada ya uchunguzi wa kitabibu tuligundua jeraha hilo lilitokana na risasi.
Hata hivyo, alisema uchunguzi ulionyesha risasi hiyo haikuvunja mfupa wa mguu wake.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daud Ntibenda, akizungumzia na maofisa
watendaji wa kata, mitaa na wenyeviti wa serikali za mitaa hivi
karibuni, alisema amesitisha utoaji wa silaha hadi zoezi la uhakiki
utakapokamilika.
Alisema wakazi wengi jijini hapa wamemilikishwa silaha kwa kudanganya kwamba ni wafanyabiashara ya madini.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia