BREAKING NEWS

Friday, April 29, 2016

UVCCM:SUMAYE ACHA KUMSUMBUA RAIS MAGUFULI

Na Woinde Shizza, Kilimanjaro

Umoja wa vijana wa Chama cha mapinduzi umemtaka Waziri mstaafu Frederick Sumaye hana vigezo wala sifa zozote zinazoweza kumfanya awe na uwezo wa kumkosoa Rais Dk John Magufuli katika uendeshaji wa serikali na masuala ya utawala. 

Sumaye ametakiwa amuache Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Magufuli ili atimize majukumu yake kwasababu alipewa dhamana ya kuwa Waziri mkuu lakini hajufikia hata thukuth ya utendaji unaofanyika sasa.   

Msimamo huo umetolewa jana na Kaimu katibu mkuu wa uvccm shaka hamdu shaka alipokuwa akizungumza na wanachama wa ccm wa kata mbili za kwandele na mbichi jimbo Rombo mkoani kilimanjaro.

Shaka alisema anachokifanya sumaye na baadhi ya wanasiasa muflis wanaojaribu kukosoa utendaji katika utawala wa serikali ya awamu ya tano ni kutaka nao wasikike wakidhani yale walioyafanya wakati wakiwa madarakani wananchi wameyasahau. 

Alisema kama yupo waziri mkuu ambaye ameonyesha udhaifu katika  utendaji na usimamizi wa serikaki huku akishindwa kumsaidia Rais hakuna atakayempita Sumaye. 

"Amekuwa waziri mkuu kwa miaka kumi kuliko waziri mkuu yeyote na kwa bahari mbaya sana ndiye waziri mkuu zero kuliko mwingine yeyote tokea tupate uhuru mwaka 1961 "alisema shaka. 

Aidha Kaimu huyo katibu mkuu alimuonya sumaye akimtaka aache kumfuatafuata Dk Magufuli katika mikakati yake ya kutumikia nchi na juhudi anazichukua dhidi ya mafisadi na wabadhirifu wa mali za umma nchini. 

Alisema wakati Rais Magufuli akiwa katika dhamira njema na nia ya wazi iuwatumikia wananchi kwa uadilifu, uaminifu na heshima alisema  kina sumaye na wenzake  wafumbe midomo yao na waache mara moja kumbughudhi Rais kwa ajili ya kusaka umaarufu wa kisiasa. 

"Sumaye aacha kufuatafuata Rais na kujifanya unajua wakati mambo yalikushinda wakati ukiwa PM, kama huna maneno ya kusema rudi Hanang ukalime maharage na karanga "alisema

Pia shaka aliwataka wananchi wa jinbo la Rombo kujitatayarisha ili kumpiga chini mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya chadema Joseph Selasini kwasabahu ni dhaifu na hatoshi kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo.

"Siku zake za kuitwa mbunge wa Rombo sasa zinahesabika, selasimi hajui anachokufanya wala hajali shida na matatizo yaliopo katika jimbo lake,lazima adui huyo apigiwe mwaka 2020 "alisisotiza shaka 

Akizungumza katika mkutano huo mwenyekiti wa uvccm mkoa wa kilimanjaro Juma Raib Juma aliwakanya wananchi wa kanda ya Kaskazini kuacha mara moja tabia ya kushiriki na kuchagua vyama na wagombea wa nafasi mbali mbali kwa ukabila, ujimbo au nasaba. 

Raibu alisema ikiwa wananchi wa kaskazini sasa wanaishi katika Mikao yote ya Tanania, si jambo la maana wao wakahesabiwa kama ni wabaguzi kwa misingi ya asili au ujamaa. 

"Tunachotaka kukisafanya baadhi ya wananchi wa Mikao ya Kaskazini ni kumuasi baba wa Taifa marehemu Mwalimu julius Nyerere, haiutuacha tukiwa tumegawanyika  , tumeishi miaka yote hatukuongozwa kwa ukabila au udini, chadema acheni kwasabahu hilo ni baa au janga katika jamii "alisema Raib. 

Jumla ya wananchi wapya 103 wa ccm na jumiya zake walijiunga na chama cha mapinduzi pia shaka alipata nafasi ya kuangalia mechi ya soka kati ya timu za kata za makiidi na mahare wilaya Rombo.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates