BREAKING NEWS

Friday, April 15, 2016

MAMLAKAYA YA HIFADHI YA NGORONGORO YAINGIA MGOGORO NA WANANCHI

Na Woinde Shizza,karatu

Wananchi wa kijiji cha  Losteti  kilichopo  katika kata ya mbulumbulu
wilayani karatu mkoani Arusha wamelalamika mamlaka  ya hifadhi ya
ngorongoro kwa kitendo cha kuwanyanganya eneo lao la kuchungia  mifugo
lijulikanalo kwa jina la Olorieni lililopo ndani ya kijiji hicho.

Wananchi hao waliyasema hayo juzi wakati wakiongea na waandishi wa
habari kijijini hapo   na kusema kuwa mamlaka hiyo ya hifadhi ya
ngorongoro wamewanyanganya eneo hilo ambalo walikuwa wanatumia kama
eneo la malisho  ya mifugo yao  kwa kipindi cha muda mrefu kwani
walianza kulitumia tangu enzi za mababu zao .

Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Aron Saiteu
Alisema kuwa eneo hilo la malisho ya mifugo ni lakwao kwa mdua mrefu
lakini wanashangaa kuona hifadhi hiyo ya ngorongoro imekuja na
kuwanyanganya hali ambayo inawafanya hata wao kukosa sehemu ya kufugia
mifugo yao.

Walisema kuwa walishapeleka malalamiko mara kwa mara  katika ofisi za
viongozi wa serekali pamoja na ofisi za hifadhi hiyo lakini amna hatua
yeyote ambayo  imechukuliwa  wala kupewa majibu ambayo yanawapa
matumaini hali ambayo imepeleka wananchi hao kuumia na kukata tamaa
ndani ya nchi yao.
Kukataa tamaa huku kumetokana na wananchi hao kutoruhusiwa kujihusisha
na shughuli zozote za uzalishaji pamoja na  kutoongezeka kwa mifugo.

“unajua ndugu waandishi sisi hapa tumeanza kufuga tangu enzi za mababu
zetu lakini tunashangaa hapo juzi mamlaka ya ngorongoro inakuja na
kusema eneo ni lao kwakweli huu ni unyanyasaji mkubwa kwa sisi
wananchi ndani ya nchi yetu yenye uhuru  wa kudhamini kila
binadamu,ivi kama kweli eneo ni lao walikuwa wapi siku zote hizo mpaka
leo ndio wanakuja wanasema eneo letu la kufugia ni la kwao kwakweli
huu ni unyanyasaji  kabisa tunaomba ndugu magufuli atusaidie
kutuangalia sisi wafugaji wa kata ya mbulumbulu” alisema Lomani Sabaya

Aidha walisema kuwa pindi wanapopeleka mifugo yao eneo hilo ata kwa
bahati mbaya upigwa faini ya shilingi 10000 kwa kila ng’ombe mmoja  na
iwapo wakikataa mmiliki wa mfugo huo uliokamatwa upelekwa mahakamani .

Akijibu tuhuma hizo kwa njia ya simu mkuu wa idara ya uhifadhi ambaye
  pia ni kaimu muhifadhi mkuu  wa mamlaka ya ngorongoro    Izrael Namani
alisema kuwa ni kweli eneo hilo ni la hifadhi hiyo ya ngorongoro
nanikweli lina mgogoro  mkubwa na wananchi wanao zunguka eneo hilo kwa
madai kuwa eneo hilo ni la kwao kwa ajili ya ufugaji kwani walianza
kulimiliki tangu enzi za mababu zao

Alisema kuwa mgogoro huu ni wa siku nyingi na unajulikana na serekali
ya wilaya pamoja na ofisi ya ardhi   na mpaka sasa ofisi ya ardhi walishazungumza na wapo kwenye harakati za upimaji na kumilikishwa
kisheria eneo hilo kwa mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro.

“unajua eneo hili linamipaka sasa tatizo kubwa lipo kwenye mipaka
wananchi wa eneo hilo hawakubali  mipaka iliopo  tatizo ndio linakuja hapa
sasa sisi mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro tulishaenda wizarani kwani
muhifadi mkuu alishaagiza   maeneo yote yeyenye migogoro  yapatiwe
ufumbuzi kwa kupimwa na kumilikishwa kisheria na uzuri watu wa wizara
ya ardhi wameshakuja na mpaka navyoongea na wawe zoezi limeanza ila
wameanzia  uko meatu ambapo napo kunatatizo kama hili na wakitoka hapo
wanakuja huku kwetu kwa ajili ya kupima na kujua mipaka hiyo ,sasa tatizo linalokuwepo apa ni kwamba  pamoja tulifanyia kazi swal ahili lakini  awa wananchi wanaona kama
sisi atulifanyiii kazi kwa  wakati ila sisi wenyewe tunatamani sana mgogoro huu uishe mapema kwakweli” Israel
Naman

Aliwataka wananchi kuwa wavumilivu wakati tatizo hili likiwa
linashughulikiwa ili kupatiwa ufumbuzi na wao kuwa walinzi wa
rasilimiali za asili kwa sera ya ujirani mwema.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates