Kaimu katibu mkuu wa UVCCM taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa anapanda mti nje ya ofisi ya CCM wilaya ya Mwanga
kaimu katibu mkuu UVCCM taifa akiwa anaongea na wananchi wa kata ya Kileo iliopo ndani ya Wilaya ya Mwanga
kaimu katibu mkuu UVCCM taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa anamkabidhi kiongozi wa timu ya Kileo jezi ambazo UVCCM mkoa wa Kilimanjaro waliaidi timu
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa kilimanjaro Juma Raibu
Juma akiwa anapanda mti wa ukumbusho nje ya ofisi ya CCM wilaya ya mwanga
Shaka akiongea na wanachama wa CCM wilaya ya Mwanga hii leo
Na Woinde Shizza, Mwanga
Wanachama wa chama Mpinduzi wilaya ya Mwanga mkoa kiliimanjaro
kimesema pamoja na kupita kimbunga cha siasa za maji taka zilizosheheni ushabiki , ubabaishaji na hujuma wana ccm wilayani hiyo wamebaki
wamoja bila kuyumbishwa na wanasiasa wasaka madaraka kwa njia za hila na
fedha .
Pia wanachama hao
wamesema kuwa wale wote
ambao walifuata siasa za ushabiki
kwa kushabikia mambo bila kupima uzani wa siasa na ubora wa kila
chama sasa hivi wako katika dimbwi la majuto na fedheha kwani wameshaona hasara za kuhama chama hicho.
Hayo yasemwa leo na
Katibu wa CCM wilaya ya Mwanga Mkoa kilimanjaro Mwanaidi Hussein Misha
wakati akitoa neno la shukran mara baada
ya Kaimu katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu
Shaka kuzungumza na viongozi wa vijiji na kata pamoja na wanachama wa chama
hicho wilayani Mwanga mkoani hapa.
Mbisha alisema umadhubuti waCCM usichukukiwe kama janbo jepesi na rahisi
badala yake viongozi wa upinzani na wanachama wanaoshabikia vyama hivyo
wakubali ukweli kuwa ccm ni zaidi mbuyu mnene wa karene ulio imara.
Alisema CCM iliioachwa na marehemu baba Taifa Mwalimu julius
Nyerere , mzee Abeid Karume., mzee Rashid Kawawa na mzee Thabit Kombo itabaki
bkuwa kimbilio na tarajio la wananchi katika kufanikisha masuala yao kisiasa,
kijamii na kiuchumi.
"Shaka nimekuwa nikikusikiasikia tu na kukusoma katika
vyombo vya habari,wewe bado kijana mdogo ila unatosha kubeba hata dhamana
kubwa., endelea mungu atakisaidia uthibitishwe kuwa Katibu mkuu "alisema
mbisha.
Akizungumzia kimbunga na bhamkani za kisiasa wakati qa
uchaguzi miuu, katibu hiyo wa wilaya aliwasifu sana wanachama wa CCM , viongozi
wastaafu, wazee, wanawake na vijana kwa
kushikamana pia kupambana toka mwanzo
hadi mwisho..
"Mayowe na kelele za wapinzani zimepotea angani, sasa
wote kimya, wanatamani kurejea ccm
wanaona aibu,hapana waambieni tu waje chama kitawapokea,hata waliotaka urais
kama wamejirudi waje nyumbani kwao "alisema Mbisha.
Awali Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa kilimanjaro Juma Raibu
Juma aliisifu wilaya ya mwanga kwa kuendelea kuwatoa mchanga wa macho kwa
kuilinda jimbo hilo lisichukuliwe na upinzani.
Raibu alisema heshima ya wana mwanga kwa ccm itaendelea
kuenziwa na kukumbukwa kika wakati kwasababu ni watu jasiri wenye msimamo
thabiti.
"Unapokuwa vitani halafu wapiganaji wako wakakataa
katakata kupokeabhongo toka kwa maadui, wakasema hatutaki na hatujunaki
chochote , hao nibwazalendo na waakinifu kama wana mwabga"alisema Juma
Hata hivyo Mwenywkiti huyo wa UVCCM mkoa wa Kilimanjaro alimpongeza Kaimu
katibu mkuu shaka kwa uthubutu wake wa kupania kurudisha heshima na hadhi ya
UVCCM iliyokuwa inapotea
Shaka anaendekea na ziara yake katika wilaya ya Same ambako
atajitimisha katika mkoa kilimanjaro kabla ya kuanza mkoani Tanga kwa siku sita
baadae Mikao ya Manyara,Kilimanjaro nq Arusha
itafanya majumuisho ya pamoja mkoani mkoani hapa.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia