Na Woinde Shizza,Arusha
Baadhi ya walimu wa jiji la Arusha wamelalamikia utaratibu uliotumika wa
upandishwaji wa madaraja na kusema kuwa utaratibu huo ni ujawatendea haki
walimu waliofanya kazi kwa kipindi kirefu pamoja na wale ambao wamestaafu .
Walimu hao walisema kuwa utaratibu uliotumika wa
kuwachanganya walimu waliofanya kazi kwa
kipindi cha mda mrefu zaidi ya miaka 20
pamoja na walimu wageni ambao wengine hawana mda mrefu kazini kwani wamefanya kwa zaidi ya mwaka mmoja hadi
miaka mitatu ni mbovu na unawakatisha tama ya kufanya kazi kwa umakini.
Mmoja wa walimu hao aliyejitambulisha kwa jina la Mark
Mbwabwo alisema kuwa mfumo huo wa
upandishwaji wa madaraja haukuwatendea haki kabisa walimu ambao wamefanya kazi kwa kipindi
cha mda mrefu kwani katika swala la ulipwaji mshahara mnakuta mwalimu aliefanya
kazi kwa kipindi cha miaka 20 analipwa sawa na mwalimu ambaye amefanya kazi kwa
kipindi cha mwaka mmoja au mitatu.
Gazeti hili lilitembelea ofisi ya chama cha walimu (CWT) mkoa wa Arusha ili kujua kama wamepata malamiko hayo ambayo
yalitolewa na baadhi ya walimu ambao wamepandishwa madaraja na kukutana na
katibu wa chama cha walimu Halmashauri ya jiji la Arusha
Magreth Hovokela ambapo alitolea ufafanuzi
tuhuma hizo na hatua ambazo wao kama chama cha walimu
wamezifikia.
Katika ufafanuzi wake alisema kuwa swala la upandishwaji wa
madaraja kwa walimu waliogota ni la mda
mrefu kwani wao kama CWT walipeleka
pendekezo hilo tangu December 17 mwa ka 2014
na serekali ikakubali kupandisha walimu waliogota kwa kipind cha muda
mrefu , serekali ilisema kuwa walimu hao wanaopandishwa madaraja wapandishwe
kutokana na muundo wa zamani ambapo ilipitishwa walimu wapandishwe kuanzia
mapema July 1 ,2015 lakini swala hilo halikutekelezeka.
Aidha aliongeza kuwa swala hilo alikutekelezwa kwa kipindi
hicho na lilianza kutekelezwa rasmi January 1 hadi machi mwaka huu na kila halmashauri imeshaanza kutekeleza
swala hilo kutokana na ilivyojipanga pamoja na bajeti yake na katika barua ambazo walimu wamepewa
za kupandishwa madaraja zinaainisha kuwa walimu hao wamepanda madaraja kuanzia
January 1 mwaka huu badala ya July 7,2015 kama vile waraka unavyoelekeza.
“sasa tatizo ambalo linalalamikiwa hapa ni kwamba walimu
ambao wamefanya kazi kwa muda mrefu wamepanda madaraja sawa na walimu ambao
wameanza kazi hivi karibuni ,kwa mfano mwalimu ambaye alikuwa ngazi ya
TGTS E₆ amepanda na
kupandishwa TGTS F₆ huku alikuwa TGTS E₆ ambaye amefanya kazi kwa miaka mingi
ameunganishwa na Yule ambaye anaanza kazi na wote kupewa kundi moja ambalo ni
TGTS F₁ kitendo ambacho kimewavunja moyo walimu waliokaa kazini mda mrefu “alisema Magreth
Aliongeza
kuwa mbali na changamoto hiyo pia
muongozi huo wa upandishwaji vyeo vya walimu wa mwaka 2015-2016 ulieleza kuwa mwalimu
ambaye amekaa kazini kwa kipindi cha mda mrefu na anakaribia kustaafu apewe
kipaumbele kwa kupandishwa vyeo pamoja na mshaara ili anapostaafu astaafie kwenye
mshahara mpya unaoendana na daraja alilopandishwa jambo ambalo halikutekelezeka
hadi baadhi ya walimu kustaafu bila kupandishwa madaraja na wamestaafia
mshahara wa zamani.
“ napenda kutumia fursa hii kuiomba serekali wawape wastaafu haki yao katika madaraja walikuwa wanastaili
kupanda ili kwani hawajachelewa maana hadi hivi sasa walimu waliostaafu
hawajalipwa mafao yao ,kwaiyo nivyema wawapandishe madaraja ndipo waweze
kuwapatia mafao yao “alisema Magret
Magret aliongeza kuwa katika halmashauri ya
jiji la arusha kuna jumla ya walimu wastaafu 18 ambao walitakiwa kupandishwa
madaraja lakini hawajapandishwa hadi kupelekea ukomo wa ajira zao serekalini.
Kwa kuwa hii
ni serikali ya awamu ya tano ya hapa
kazi tu chama cha walimu na walimu kwa ujumla wanayoimani kubwa kwa kuwa
maswala yao sasa yatashulikiwa kwa wakati .