TIGO YATOA MSAADA WA MADAWATI 235 KWA SHULE ZA MSINGI MKOANI KAGERA

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Deodatus Kinawiro akipokea msaada wa madawati 235 kwa mkoa wa Kagera toka kwa Meneja wa Tigo kanda ya ziwa , Edgar Mapande jana kwenye shule ya msingi Katoro wilayani Bukoba

Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Vijijini  Deodatus Kinawiro akihutubia wakazi wa Bukoba baada ya makabidhiano ya madawati 235 kwa shule za msingi Kagera makabidhiano hayo yalifanyika katika shule ya msingi Katoro wilayani Bukoba 


 Meneja wa Tigo kanda ya ziwa , Edgar Mapande  akitoa hotuba kwa wageni waalikwa na wanafunzi mara baada ya makabidhiano ya madawati 235 kwa shule za msingi za mkoa wa  Kagera ,katika hafla iliyofanyika katika shule ya msingi Katoro wilayani Bukoba.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Katoro wilayani Bukoba wakishuhudia makabidhiano  ya madawati 235 kwa shule za msingi mkoani Kagera   toka kampuni ya simu za mkononi Tigo.


Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Katoro wilayani Bukoba wakiwa wameketi kwenye moja ya dawati kuonyesha kuwa wamepokea madawati toka kampuni ya simu za mkononi Tigo.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

إرسال تعليق

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia