“Vinywaji vyenye kemikali hatari kwa afya – Dkt Kazoba”
Na Woinde Shizza , Arusha
Jamii imeaswa kuhakikisha kuwa wanatumia vinywaji vya asili ambavyo havina kemikali Kali ili kuweza kutunza kinga ya mwili
Hayo yameelezwa na Dkt Mwesiga Kazoba Ambaye ni mkurugenzi wa taasisi ya kizoba herbal clinic Wakati akiongea na waandishi kwenye maonesho ya biashara(saba Saba) Dar es salaam
Kazoba alisema kuwa vinywaji venye kemikali Kali vina madhara makubwa sana Kwa afya lakini Kwa sasa tayari mbadala wa Hilo wameshaupata.
Alisema kuwa kutokana na Hilo sasa wameamua kuboresha vinywaji ambavyo mara nyingi vinatumiwa na vijana ambapo Wana kinywaji ambacho pia ni kiburudisho Kwa mtumishi
"Sisi tumekuja na kinywaji aina ya energy drink ambayo inaitwa kazoba natural energy drink tumetumia biadha za kitamaduni hakina kilevi na tunataka tuenzi hata vyakwetu"
Wakati huo huo kazoba alisema kuwa yeye kama mtafiti wa madawa ya asili,pia amefanikiwa kupata suluhisho hasa la tatizo la mgongo kwa kuwa tatizo Hilo limekuwa likiwasumbua watu wengi
"Tupo na suluhisho la matatizo kama vile mgongo unajua watu wanaokaa muda mrefu,au wanafanya kazi muda mrefu pia wanapata changamoto hiyo sasa basi suluhu ya Hilo tumepata"aliongeza
Alihitimisha kwa kusema kuwa tiba pamoja na madawa ambayo wanatoa Kwa wagonjwa yamesajiliwa na kutambulika kutoka Kwa mamlaka husika ivyo basi wananchi wanatakiwa kuwa na imani na biadhaa zake.
Naye msemaji wa kampuni hiyo Bi Theodora Mrema alisema kuwa Miongoni mwa faida kwa mtumiaji wa kinywaji hicho ni pamoja na kuondoa sumu mwilini,kuboresha mzunguko wa damu,kuondoa uchomvu kuyeshusha chakula pamoja na kupandisha kinga za mwili
Theodora alisisitiza umuhimu wa watu kutumia vitu vya asili ,huku ujio wa kinywaji hicho akisema ni mkombozi kwa watakaokitumia Kwa kuwa hakina kemikali yoyote.




0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia