Picha na Michael Nanyaro |
Mahakama ya hakimu mkazi Arusha wamesikiliza shauri la watuhumiwa 61 wa makosa ya ugaidi chini ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Nestory Baro Na mwendesha mashtaka wa serikali Grace Madikenya.
Picha na Michael Nanyaro |
Watuhumiwa hao walifikishwa kwenye viwanja vya mahakamani hapo Majira ya saa 9:27 na gari la magereza lenye mamba MT0040 tukio lililo ambatana na baadhi ya mahabusu 29 kugoma kushuka kwenye basi na wengine 32 kuitikia agizo la mahama la kwenda kusikiliza mashauri yao .
Picha na Michael Nanyaro |
Tukio
hilo la kugoma kwa watuhumiwa hao kushuka kwenye basi kumepelekea kusimama kwa
shughuli za mahakama kwa zaidi ya saa moja ili kutafuta njia sahihi ya kutatua
tatizo hilo.
Wakizungumza
mahakamani hapo watuhumiwa 32 waliopanda kizimbani walisema kuwa wamehamua
kuitikia agizo la mahakama kutokana na barua iliyotoka kwa mkuu wa upelelezi wa
Mkoa (RCO) kuwa Madai yao yamefanyiwa kazi ambapo aliwataka kusitisha mgomo.
"Tumekuja
mahakamani kusikiliza nini walichotuitia ili tujue wapi mahakama walipofikia
kwenye upelelezi wao laki cha kusikitisha mambo ni Yale Yale ya kupigwa tarehe
kutokana na hali hiyo hatutakuja tena maana tumecho kuzungushwa"
Wameitaka
mahakama kuwaacha mahabusu mpaka upelelezi wao utakapo kamilika kwa sababu
shauri lao lina muda mrefu tangu mwaka 2014 bila kufanyiwa kazi.
Walitaka
kujua mashauri yao ni namna gani yamefanyiwa kazi ili kujua kesi yao ilipofikia
na hakimu atakayesikili
"Tupo
tayari kufungwa kama kweli tunamakosa tunasikitishwa na upande wa upelelezi
kushindwa kufanya kazi yake kwa wakati kama wameshindwa kupata ushaidi wa
kuthibitisha tuhuma hizo basi waachiwe huru
Walisema
mgomo huo utaendelea mpaka upande wa jamuhuri utakapokuwa tayari kuwasomea
mashtaka au kuwaachia huru.
Akijibu
Madai hayo hakimu mkazi wa mahakama hiyo Nestory Baro alisema kuwa mkuu wa
kitengo cha upelelezi Mkoani hapa umeshakamilisha uchinguzi wao na majalada
wamepeleka makao makuu ambapo amehairisha shauri hilo adi mei 8 mwaka huu.
0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia