NASSARI ACHAGULIWA KUWA MGOMBEA UBUNGE CHADEMA AWAPITAWAGOMBEA WENGINE KWA KURA 805
Nassari akiwaanashangiliwa na wananchi wajimbo la Arumeru Mashariki mara baada ya kupita kwenye kinyanganyiro za kumtafuta mgombea anaegombea kwakupitia chama hicho
Wananchi wakiwa wanamshangilia mgombea ubunge aliyepita kupitia chaa cha demokrasia na maendeleo Chadema Joshua Nassari aliyekaa juu ya gari
HATIMAYE chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)Kwa jimbo la
Arumeru kimefanikiwa kupata mgombea ubunge,Joshua Nassari ambapo
amefanikiwa kupata kura 805 sawa na asilimia 90.6 ya kura 888.
Akitangaza matokeo hayo kamanda wa oparesheni ya uchaguzi taifaBw
John Mrema alisema kuwa Mgombea huyo amepata kura nyingi sana na
kuwaacha wagombea wenzake saba akiwemo aliyehama chama cha mapinduzi
baada ya kuambulia kura 22 kwenye kinyang’anyiro cha kura za maoni.
Bw Mrema aliwatanga wagombea wengine kuwa ni pamoja na Bi Anna Mbwira
ambaye alipata nafasi ya pili kwa kura 25 sawa na asilimia 2.56 wakati
wa tatu ni Bi Rebecca Magwisha ambaye alipata kura 12 sawa na asilimia
1.4
Wengine ni Bw Samwel Shami ambaye naye aliambulia kura 10 sawa na
asilimia 1.1 wakati Mgombea Anthony Musani alipata kura 8 sawa na
asilimia 0.9 na nafasi ya mwisho ilishikwa na Yohana Kimuto ambaye
alifanikiwa kupata kura 6 sawa na asilimia 0.6
“kwa sheria iliopo na kwa mujibu wa matokeo haya ambayo pia kura sita
ziliharibika sasa namtangaza Bw Nassari kuwa ndiye atakayetuwakilisha
katika uchaguzi wa jimbo letu la Arumeru Mashariki kwa hivyo
ushirikiano ni muhimu sana””alisema Bw Mrema.
Pia katika Matokeo hayo wagombea wote sita ambao walishindwa katika
mchakato huo walisema kuwa kwa sasa wana nafasi kubwa sana ya kuweza
kusaidiana ili jimbo liweze kurudi ndani ya chama hicho kwa kuwa wana
uwezo wa kuwa na mgombea ndani ya chama hicho.
Akiongea mara baada ya kushindwa katika mchakato huo lakini bado ana
nafasi kubwa sana ya kuweza kuelezea umma juu ya chama cha mapinduzi
kwa kuwa chama hicho mara nyingi sana kimeonekana kukuika hata
maadili ya mtanzania
Bw Musani alisema kuwa bila kuogopa kitu chochote hataelezea hadharani
maovu ya CCM ambayo yanafanyika ikiwa ni pamoja na kufichua mbinu
mbalimbali ambazo zinafanywa na chama hicho hasa katika nyakati za
uchaguzi.
Kwa Upande wake Katibu mkuu wa chama hicho cha chadema Dkt Wilboard
Slaa alisema kuwa mpaka sasa kutokana na vijiji 86 kuikubali Chadema
ni wazi kuwa jimbo hilo lipo kwao kwa maana hiyo wanasubiri kumupisha
Bw Nassari
Dkt Slaa alisema kuwa mpaka sasa chama chake kimejiwekea utaratibu
ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa wanachafua hali ya hewa ndani ya
jimbo la Arumeru Mashariki, ambapo kila nyumba itapepea bendera ya
Chadema.
“”Nitahakikisha kuwa ili zoezi linaenda vema na pia msije mkaja kwangu
mkasema kuwa mmeibiwa kura mimi sitaweza kuwasikiliza ila nitawauliza
maswali hakikisheni kuwa hamuibiwi kura na kila nyumba inatakiwa
kuppeea bendera ya Chadema tena mpya kabisa na mimi nitasimamia hili
zoezi”alisema Dkt Slaa.
Naye Mshindi ambaye ni Nassari alisema kuwa mara baada atakapoingia
Bungeni atahakikisha kuwa anarudisha ubunge kwa wanananchi ikiwa ni
pamoja na kujinyima hata kwa posho zake ili kuwarudishia wananchi
maendeleo.

habari hii imeandikwa na Pamela Mollel wa libeneke la kaskazini

0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia