VIJANA WATAKIWA KUTHUBUTU ILI KUJILETEA MAENDELEO
Waziri
wa Habari Vijana,Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dk Fenella Mukangara
akizungumza na washiriki wa kambi ya vijana leo jijini Dar es Salaam
alipokuwa akifungua rasmi kambi hiyo ambayo imeanza tarehe 29 na
inatarajiwa kumalizika tarehe 2 Agosti.Kambi hiyo ya vijana ya Dunia
imeandaliwa na taasisi isiyo ya Kiserikali International Youth
Fellowship(IYF) kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo.


Baadhi
ya washiriki wa kambi ya vijana wakisikiliza hotuba ya Mheshimiwa
Waziri Fenella Mukangara hayupo pichani alipokuwa akifungua rasmi kambi
hiyo leo jijini Dar es Salaam.


Kikundi
cha sanaa kutoka IYF wakicheza muziki wa kitamaduni kutoka Korea mbele
ya mgeni rasmi Waziri wa Habari Vijana,Utamaduni na Michezo Mheshimiwa
Dk Fenella Mukangara wakati wa hafla ya ufunguzi kambi ya vijana leo
jijini Dar es Salaam.

Waimbaji
wa Kwaya ya kimataifa kutoka Korea Gracias wakiimba wakati wa hafla ya
ufunguzi wa kambi ya vijana l;eo jijini Dar es Salaam.

Kikundi cha sanaa kutoka Tanzania wakionyesha mchezo wa Tai Kondo leo jijini Dar es Salaam.

Waziri
wa Habari Vijana,Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dk Fenella Mukangara
akiteta jambo na Mkurugenzi wa IYF Tanzania Pastor Joen Hee Yong
(katika) kushoto ni mwanzilishi wa IYF Duniani Pastor Park Ock Soo.

Waziri
wa Habari Vijana,Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dk Fenella Mukangara
akifurahia kwaya ya Gracias ilipokuwa inaimba wimbo wa Taifa wa Tanzania
kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Tanzania Profesa Elisante
Ole Gabriel.
PICHA ZOTE NA Frank Shija - Maelezo


0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia