MOTO MKUBWA WATEKETEZA UWANJA WA NDEGE WA JOMO KENYATTA NCHINI KENYA

Moto mkubwa unaripotiwa kuzuka asubuhi hii katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyetta (JKIA) jijini Nairobi.
Chanzo cha moto huo bado hakijatambulika na juhudi za kuuzima
zinaendelea, ambapo vikosi mbalimbali vya zimamoto vipo uwanjani hapo
kuthibiti janga hilo.


Uwanja huo hivi sasa umefungwa na hakuna ndege kutua ama kuruka isipokuwa kwa dharura tu.
Moto huo unasemekana ulianza majira ya saa 11 za alfajiri sehemu za
idara ya uhamiaji na kusambaa katika eneo la abiria wa kimataifa.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya anaripotiwa kuelekea uwanjani hapo hivi
sasa kukagua janga hilo, na habari zinasema hakuna mtu aliyedhurika kwa
moto huo ingawa hasara iliyopatikana inasemekana ni kubwa na kwamba
abiria wengi wamekwama uwanjani hapo. Barabara kuu ya kuelekea JKIA
imefungwa
0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia