WATANZANIA JIAJIRINI MSIKUBALI KUAJIRIWA

Vijana na Watanzania kwa jumla wameaswa kuacha kutegemea ajira za ofisini, badala yake watafakari namna ya kujiingiza katika ujasiriamali ili kuondokana na umaskini. 

Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Kitivo cha Elimu ya Biashara na Uchumi wa Chuo Kikuu cha Iringa (IUCo), Enock Ugulumo wakati alipokuwa akizungumza kwenye maadhimisho ya wiki ya ujasiriamali iliyofanyika kwenye viwanja vya chuo hicho mjini Iringa.
Maadhimisho hayo yalilenga kuwaongezea vijana na wanafunzi wa chuo hicho maarifa katika kujitegemea. Utafiti wa wataalamu mbalimbali duniani unaonyesha asilimia kubwa ya watu wanaogemea ajira hufa wakiwa maskini, tofauti na wale wanaojiajiri.

Alisema chuo hicho kimeanzisha mpango huo chuoni hapo ili kuibua vipawa vya vijana na kuwawezesha wanafunzi kutumia elimu na ujuzi walionao kuibua ajira mpya, hatua itakayotoa fursa kwa jamii kupata nafuu ya upatikanaji wa kazi.
“Mfumo huu wa ujasiriamali ambao unaendana na mafunzo kwa vitendo, umelenga kuwafundisha wanafunzi namna ya kutengeneza bidhaa na kutoa huduma, kama sehemu ya kukabiliana na tatizo la ajira”.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kitengo cha Ujasiriamali wa Chuo hicho Dk Hosea Mpogole alisema mpango wa ujasiriamali kwa wanafunzi ulioanzishwa chuoni hapo utapunguza kero ya upatikanaji wa ajira nchini.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia