Afisa wa bima kutoka mamlaka ya usimamizi wa Bima Arthur Mbena
aakiwa anatoa maelekezo ya mafunzo kwa afisa wa polisi kitengo cha
usalama barabarani mkoa wa Arusha pamoja na wananchi waliofika eneo hilo
jinsi ya kuhakiki Bima yake ya chombo cha moto ni halali au bandia ni
halali au ni bandia ,huu ukiwa ni mfumo mpya unaotumia simu ya mkononi
au tovuti uliozinduliwa leo ndani ya jiji la Arusha ambapo
utasaidia wananchi kuepuka kuuziwa bima feki za vyombo vyao vya moto
kamishina wa mamlaka ya
usimamizi wa bima nchini Dkt.Baghayo
Abdalah Saqware akiwa anaongea na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua mfumo wa kudhibiti udanganyifu katika bima za vyombo vya moto (TIRA MIS)
meneja wa Mamlaka ya usimamizi wa Bima wa kanda ya kaskazini Elieza Roikiza akiwa anamuelekeza
mwananchi jinsi ya kuhakiki bima ambayo sio fek i
kamishina wa mamlaka ya
usimamizi wa bima nchini Dkt.Baghayo
Abdalah Saqware akiwa anawaelekeza baadhi ya maaskari wa usalama barabarani jinsi ya kuhakiki bima feki na ambayo sio feki
wamiliki wa bima wakiwa katika uzinduzi
Na Woinde Shizza,Arusha
Zaidi ya kesi 10 za
kughushi nyaraka za bima zimefikishwa mahakamani katika kipindi cha miaka mitatu na kati ya
kesi hizo watu watano wamehukumiwa kwenda jela
na mashauri matatu yakiwa
yamekatiwa rufaa katika mahakama kuu huku watu wawili wakiwa wameamriwa kulipa faini.
Akiongea katika uzinduzi
wa kampeni ya kuthibiti
udanganyifu katika bima za vyombo vya moto
(TIRA MIS) kamishina wa mamlaka ya
usimamizi wa bima nchini Dkt.Baghayo
Abdalah Saqware alisema kuwa kumekuwa na
wimbi kubwa la udanganyifu katika soko la bima
linalohusisha utengenezaji na uuzaji wa stika na hati za bima
bandia hivyo wameamua kuanzisha kampeni
hii ili kuweza kumaliza kabisa tatizo hili.
Alisema kuwa mamlaka hiyo
hadi sasa imeshawakamata wahalifu 10 na kati yahao kunawalifikishwa
mahakamani na kuhukumiwa kwenda jela huku wengine wawili wakiwa wameamriwa
kulipa faiini kati ya shilingi milioni
20,000,000 hadi shilingi 40,000,000 kutokana na makosa waliyofanya .
Alisema kuwa
inakadiriwa hasara ya kiasi cha asilimia 10% ya mapato yote ya biashara ya bima ya vyombo vya moto inaingia kwenye mikono
haramu ikiwa ni pamoja na wimbi la
kughushi nyaraka za bima kuongezeka ,huku uhalifu wa usafirishaji wa magari
yanayopitia bandari zetu na kupele nchi
jirani (IT) pamoja na ule wa bodaboda unachangia kwa kiasi kikubwa .
“stika hizi bandia zimekuwa zikichapishwa na watu wasio kuwa
waaminifu na kusababishia hasara kubwa mawakala wa bima na makampuni ya bima
kwa kuwapoteze mapato ambayo ndio hutumika kulipa hasara na majanga yanapotokea
,kutokana na haya yote mamlaka sasa
imeamua kutafuta njia mbadala kwa kutumia TEHAMA ili kuondoa tatizo hili kwa kumuwezesha mkata
bima kuhakiki taarifa za bima yake kwa kutumia teknolojia rahisi ambapo mamlaka
imeanzisha mfumo huu utakaotumika
kuhifadhi na kuhakiki taarifa za bima za
vyombo vya moto “alisema Dkt.Baghayo
Kwa upande wake meja wa kanda wa Mamlaka ya usimamizi wa bima Elieza Roikiza alisema kuwa utengenezwaji wa mfumo huu umetokana na uwepo wa bima bandia za vyombo vya moto kama magari
,pikipiki na aina zinginezo za vyombo vya moto hivyo wanaamini kabisa mfumo huu
wa moto utakuwa rafiki sana kwa wanachi,na pia utamuwezesha mwananchi yeyote
popote alipo Tanzania kuhakiki bima ya chombo chake kwa kutmia njia mbili za
urahisi ambazo ni simu yake ya mkoni
pamoja na kufungua tofuti ya mfumo huu
Alisema kuwa mfumo huu utasiadia kuondoa stika na hati za bima
bandia,utarudisha imani ya wananchi
katika huduma za bima nchini,pia
itaongeza idadi ya vyombo vya
moto vinavyokatiwa bima pamoja na itaiongezea mapato serikali yanayotokana na ushuru pamoja na kodi inayotozwa katika bima za
vyombo vya moto.