UZINDUZI RASMI WA KAMPENI ZA CHADEMA KWA UDIWANI WA KATA NNE ZA ARUSHA; CHADEMA WATUMIA CHOPA NA KUSISITIZA AMANI NA HAKI VITAWALE
Akizungumzia chaguzi hizo, Mh Lema aliwatahadharisha viongozi wa Mkoa, Wilaya na Jeshi la Polisi kutojaribu kuingilia chaguzi hizo. Akadai kuwa akionewa mmoja watakuwa wameonewa watu wote na hivyo hawatakubali.
Aidha, Lema alizungumzia ‘msuguano’ wa udini nchini, na kusema kuwa suluhisho haliwezi kupatikana kwa kufanya propaganda. Alidai kuwa suluhu itapatikana kwa pande zote zinazohusika, akitaja Serikali na viongozi wa dini zote kukaa pamoja na kuelezana ukweli ili kupata suluhu ya kudumu. Lema alidai kamwe hataacha kusema ukweli kwa kuogpa kukosa kura kama wengine kwa kuwa kiongozi wa kweli hasemi uongo ili apate kura.
Mh Lema amezungumzia pia tuhuma dhidi yake na chama chake kuwa wanapenda fujo na maandamano, na kukanusha huku akifafanuo kuwa sio kweli kwamba wanapenda fujo na maandamano, bali hawapendi na hawakubali kuonewa au kudhulumiwa haki zao.
Mbunge huyo alifichua pia tuhuma za ufisadi mkubwa aliodai kuugundua kufanywa na Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Nanyaro amewaeleza maelfu ya wananchi waliojitokeza viwanjani hapo kuwa wao kama Chadema hawaendi kushiriki uchaguzi, bali kushinda na kurudisha Kata zao ambazo ziliachwa wazi baada ya chama chake kuwafukuza madiwani waliowakilisha Kata hizo kwa alichodai ni kupokea rushwa ili wahujumu Chadema katika sakata la kutafuata muafaka wa uchaguzi wa Meya waliodai kuwa batili na baadae kupelekea vifo vya watu watatu na makumi wakiwaki na mejeraha na wengine ulemavu.
Akisisitiza zaidi, Bw Nanyaro amedai kuwa lengo la Chadema ni kuzirudisha Kata hizo ili wapate nguvu ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Meya Gaudence Lyimo ili uitishwe uchaguzi upya. Alidai kuwa kwasababu Tume ya Uchaguzi imeonekana kumtambua aliyekuwa diwani wa kata ya Sombetini (Alphonce Mawazo aliyehamia Chadema toka CCM), basi wao Chadema watamuita Mawazo ahudhurie vikao vya Halmashauri kama awali, akiwa mwakilishi wa CCM lakini akifanya kazi ya Chadema.
Nae Katibu wa Chadema Wilaya ya Arusha Mjini Bw Martin Sarungi alipopewa nafasi ya kuongea alitumia nafsi hiyo kutahadharisha kwamba Chadema kupitia intelijensia yao wamegundua mbinu ovu za makusudi kuvuruga mikutano ya Chadema katika Kata tofauti kwa kuansiha vurugu ama kurusha mawe.
Sarungi aliwataka wapenzi wote wa Chadema kuwa walinzi wa amani katika mikutano yao yote ya Chadema na kwamba yeyote watakayemtilia shaka nataka kuvuruga amani watoe taarifa ama kumfikisha kwenye vyombo husika.
About Woinde Shizza
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia