MAPOKEZI YA DK. KAFUMU IGUNGA YAFUNIKA
Posted by
woinde
on
Monday, May 13, 2013
in
|
*MAELFU WAJITOKEZA KUMLAKI
*CCM YAAHIDI KUTEKELEZA AHADI ZOTE KABLA YA 2015
*NAPE ATAKA VYAMA VYENYE MLENGO WA UGAIDI VISUWE
|
Dk. Kafumu akiwasalimia wananchi kwenye mkutano huo.
Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye |
NA BASHIR NKOROMO, IGUNGA
WAKATI
mapokezi ya Mbunge wa Igunga Dk. Dalally Peter Kafumu yamesababisha
baadhi ya shughuli kusimama, kwa hoi hoi, nderemo na vifijo, Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kimeahidi kuongeza kasi ya utekelezaji wa ahadi ilizotoa
katika jimbo hilo.
Akizungumza
kwenye mkutano wa mapokezi ya Dk. Kafumu uliofanyika leo kwenye Uwanja
wa Sokoine mjini hapa, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye,
alisema CCM lazima itazitekeleza ahadi zote zilizotolewa na mbunge huyo
kupitia ilani ya Chama wakati akigombea katika uchaguzi mdogo
uliofanyika 2011 jimboni humo.
"Baada
ya mahakama kumrejeshea Ubunge mbunge wetu, CCM inaahidi kwamba ahadi
zote alizotoa mbunge wenu zitatekelezwa kabla ya mwaka 2015. Na kwa kuwa
Chadema walipunguza kasi kwa kusimamisha mbunge wenu baada ya kumpeleka
mahakamani, CCM itaisimamia serikali ili kuhakikisha inaongeza kasi ya
utekelezaji wa ahadi hizo kufidia pale utekelezaji ulipokuwa umepungua
kasi", alisema Nape.
Alisema,
licha ya Dk. Kafumu kusimamishwa na mahakama, CCM iliendelea kutekeleza
ilani katika jimbo la Igunga, kwa sababu ni wajibu wake kutokana na
kwamba CCM ndicho chama chenye ilani inayotelekezwa kutokana na
kuvishinda vyama vyote katika uchaguzi mkuu uliopita.
Nape
alisema, moja ya miradi ambayo Dk. Kafumu na CCM waliahidi ni ujenzi wa
daraja la mto Mbutu ambalo, alisema, sasa ujenzi wake unaendelea na
yapo matumaini ya kukamilika kama ilivyopangwa.
Alisema,
ahadi zingine ni kuhusu umeme, Barabara na afya ambavyo ni miongoni mwa
mambo ambayo yapo katika ilani ya CCM, ambayo lazima CCM iyape
kipaumbele kuhakikisha yanakamilika kuondoa au kupunguza kero za
wana-Igunga.
Nape
aliwataka wananachi wa Igunga kumpokea mbunge wao kwa mikono miwili na
kumpa ushirikiano katika kutekeleza ahadi zake kwa sababu ni Mbunge
ambaye wamepewa na Mungu wao na ndiyo sababu ameweza kurejeshwa na
Mahakama licha ya juhudi za Chadema kujaribu kumkwamisha asiwatumikie.
"Hukumu
ya kwanza tulishangaa, lakini kwa sababu tuliheshimu sheria kukatulia
na kukata rufani. Mungu amekaa kati yenu wana Igunga amewarejeshea Dk.
Kafumu", alisema Nape.
Akizungumzia
hali ya kisiasa nchini, Nape aliwataka wanaigunga na Watanzania kwa
jumla sasa kuwa makini na vyama vya siasa vilivyopo hapa nchini akidai
baadhi vimegeuka kuwa vyama vya vurugu na vya kigaidi badala ya kuwa vya
siasa kama ilivyokusufdiwa.
Nape
aliwataka wananchi wa Igunga kuwatenga wanaoshabikia chama chochote
kinachoonekana kuwa cha fujo na kuwa na mipango ya kigaidi.
Akizungumza
kwenye mkutano huo, Dk. Kafumu alisema, amefarijika sana kurejeshewa
ubunge, akisema anatambua kuwa yeye ndiye chaguo la ubunge kwa wana
Igunga kwa kuwa wanamtumainia katika kushirikiana nao kwenye katika
kuliendeleza jimbo lao na Tanzania kwa jumla.
Dk.
Kafumu aliahidi kuendelea na utekelezaji wa ahadi zake alizowapa
wananchi wa jimbo hilo, ikiwemo ujenzi wa dalaja katika mto Mbutu ambalo
alisema kutokuwepo kwa daraja hilo kumekuwa moja ya voikwazo vya
maendeleo jimboni.
"Alipokuwa
nazungumza hapa (Nape) nimetamani kulia kama mtoto wa Mkulima (Waziri
Mkuu Mizengo Pinda), kutokana na hisia zilizoniingia kutokana na maneno
aliyosema. kwa hiyo sina mengi ya kusema zaidi ya kuwashukuru kwa
kunitia moyo nilipokuwa sipo kama mbunge wenu, maana nimekuta baadhi ya
ahadi zaungu zimeendelea kutekelezwa", alisema Dk. Kafumu.
"Napenda
niwahakikishieni kwamba nitatekeleza ahadi zangu zote na sina shaka
nitafanikiwa akwa kuwa mmenipa moyo mkubwa kwa mapokezi mliyonipa na
hivyo naamini mtashirikiana nami kwa nguvu zaidi kutekeleza ahadi hizo",
alisema.
Mapokezi
ya Dk. Kafumu ambaye aliwasili saa nane alasirin akitokea Dodona na
Nape, yalianzia kiasi cha kilometa tano nje ya mji ambapo ulienda kwa
kusindikizwa na pikipiki zaidi ya 200 na bajaji zaidi ya 60 huku wengine
wakitembea kwa miguu kwa shamrashamra hadi Ofisi ya CCM ya Wilaya ya
Igumnga.
Kabla
ya ubunge wake kutenguliwa na Mahkama baada ya Chadema kwenda
mahakamani, baada ya kushinda katika uchaguzi mdogo uliofanyika mwaka
2011, kufuatia aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Rostam Aziz kujiuzulu.
PICHA ZAIDI ZA MAPOKEZI HAYO:
Wananchi
wakimbeba Mbunge wa Igunga mkoani Tabora, Dk. Dalally Peter Kafumu
kumpeleka jukwaani, wakati wa mkutano wa mapokezi yake, jimboni humo
uliofanyika leo kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Igunga. Dk.
Kafumu amerejeshewe ubunge na mahakama kuu baada ya kukata rufani
kufuatia awali kuvuliwa pia na mahakama baada ya Chadema kwenda
mahakamani aliposhinda katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo uliofanyika
mwaka juzi.
Waendesha bajaji wakimsubiri Dk. Kafumu nje ya mji wa Igunga wakati walipowasili leo
Msafara wa Dk. Kafumu, ukiongozwa na pikipiki na bajaji baada ya kuwasili mjini Igunga leo
Dk. Kafumu akiwa na Nape wakati wa mapokezi hayo
Wazee wa Igunga wakimpongeza Dk. Kafumu kwa kurejeshewa Ubunge, alipowasili leo jimboni Igunga
Dk. Kafumu akisalimia na baadhi ya wanachama wa CCM alipowasili kwenye Ofisi ya CCM ya Wilaya ya Igunga leo
Dk. Kafumu na Nape wakiwapungia wananchi baada ya kuwasili Igunga
Wananchi
wakimshangilia Dk. Kafumu alipowasili kwenye mkutano wa mapokezi yake
uliofanyika kwenye Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mjini Igunga
Dk. Kafumu akiwa na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Igunga, Coasta Olomi, kwenye mkutano huo wa mapokezi
Nape akihutubia kwenye mkutano huo wa mapokezi ya Dk. Kafumu
"DC hakikisha unasimamia kwa nguvu zote ilani ya uchaguzi ya CCM hapa Igunga", Nape kimwambia mkutano Mkuu wa wilaya ya Igunga
Kila mmoja alikuwa na shauku ya kumuona Dk. Kafumu kiasi kwamba waliokosa nafasi walipanda kwenye miti kama vijana hawa.
Maelfu ya wananchji waliofurika kwenye mkutano wakishangilia
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia