Askari wa jeshi la magereza wakionyesha uhidari wao katika gwaride, picha hii ni ya maktaba haiusiane na tukio hili.
ASKARI
magereza mwenye cheo cha Koplo amenusurika kipigo kutoka kwa wananchi
wenye hasira baada ya kubainika kuwalawiti kwa siku moja vijana wawili
wa kiume wenye umri wa kati ya miaka 18 na 20.
Tukio
la kuwalawiti vijana hao linadaiwa kufanywa na askari huyo kati ya
majira ya saa 7.00 mchana na saa 2.00 usiku katika moja ya nyumba za
kulala wageni (jina limehifadhiwa) iliyoko mtaa wa Mafisa manispaa ya Morogoro.
Akisimulia
mkasa huo, Meneja wa nyumba hiyo ya kulala wageni jina tunalo alisema
kuwa imekuwa ni desturi ya askari huyo kwenda na vijana wa kiume katika
nyumb
a hiyo hali iliyowatia wasisi wahudumu wa nyumba hiyo.
a hiyo hali iliyowatia wasisi wahudumu wa nyumba hiyo.
Alisema
kuwa siku ya tukio askari magereza huyo alifika katika nyumba hiyo ya
kulala wageni majira ya saa 7.00 mchana akiwa amempakia kijana mmoja
katika pikipiki yake na kabla ya kukabidhiwa funguo ya chumba namba 202,
mhudumu wa nyumba hiyo alimwambia askari magereza huyo kuwa masharti ya
nyumba yao hayaruhusu watu wa jinsia mmoja kukaa chumba kimoja.
Alisema
kuwa askari huyo alimtambulisha kijana aliyekwenda naye pale kuwa ni
mdogo wake na kwamba walikuwa na mazungumzo naye ya muhimu na baada ya
mazungumzo hayo kijana huyo angeweza kuondoka.
Hata
hivyo, muda mfupi baada ya watu hao kuingia chumbani mmoja wa wahudumu
alipita karibu na mlango wa chumba hicho na kusikia sauti ya mahaba,
hali iliyomtiwa wasiwasi na kulazimika kuripoti tukio hilo kwa meneja
wake.
Majira
ya saa 11.00 jioni askari huyo alitoka na kijana huyo na kuahidi kurudi
tena baadaye na aliporudi majira ya saa 1.00 usiku alirudi na kijana
mwingine anayedaiwa kuwa mwenyeji wa mkoa wa Tanga na kwa siku hiyo
alikuwa akitokea jijini Dar es Salaam baada ya kupigiwa simu na askari
huyo.
Askari
huyo alingia chumbani akiwa na kijana huyo na muda mfupi alitoka na
kwenda dukani kununua kodomu na mafuta ya mgando pasipokujua kuwa
kulikuwa na watu waliokuwa wakifuatilia nyendo zake.
Aliporudi
na kuingia chumbani baadhi ya vijana waliokuwa wameandaliwa walizunguka
nyuma ya chumba hicho na kuchungulia dirishani na ndipo walipojionea
mambo yote yaliyokuwa yakiendelea chumbani humo.
Majira
ya saa 2.00 usiku baada ya mambo hayo kumalizika kijana huyo alitoka na
kumuacha askari huyo akioga hata hivyo kabla hajafika mbali meneja wa
nyumba hiyo ya kulala wageni akiwa na wakazi wengine wa mtaa huo
walionesha kukerwa na kitendo kile walimvamia kijana huyo wakitaka
kumhoji sababu za kushiriki kitendo kile cha aibu.
Hatahivyo,
wakati wananchi hao chini ya mjumbe wa seriakli ya mtaa wa Mafisa,
Amina Mandawa, wakiendelea kumbana kijana huyo askari huyo alifika
katika eneo hilo akiwa na pikipiki yake na kujikuta akipokea kipigo
baada ya kubainika kuwa ndiye aliyekuwa akimlawiti mtoto huyo.
Kufuatia
dhahama hiyo, askari polisi wanaotumia pikipiki maarufu kama
‘Vodafasta’ alifika katika eneo hilo na kuwanusuru watu hao na kibano
cha wananchi na kufanikiwa kuwapeleka kituo kikuu cha polisi kwa
mahojiano.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, amekiri jeshi lake
kumshikiria askari magereza pamoja na kijana anayedaiwa kulawitiwa na
askari huyo kwa muda kabla ya kuachiwa kwa dhamana siku hiyohiyo majira
ya saa 8.00 usiku.
Kamanda
Shilogile alisema kuwa tayari jalada limefunguliwa na kupelekwa kwa
mwanasheria mkuu wa serikali kama ilivyo utaratibu wa sasa ambapo kesi
zote za jinai hazisimamiwi na jeshi hilo kama ilivyokuwa awali.
Habari
zaidi zinadai kuwa askari magereza huyo amehamia mkoani Morogoro miezi
minne iliyopita akitokea Arusha ambako nako inadaiwa alihamishwa
kutokana na kuwa na tabia ya kulawiti vijana wadogo.
HABARI KWA HISANI YA BERTHAMOLEL BLOG