Mh. Lowassa aipongeza kampeni ya hoteli ya Double Tree ya kutoa taa za nishati ya jua akisema kuwa ni asilimia 14 tu ya watanzania ndio wanaopata umeme

IMG_9427
Mkurugenzi wa Kanda wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton ya Dar es Salaam Bw. Judd Lehmann akifafanua jambo kwa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli Mh. Edward Lowassa (kulia) ambapo amemweleza kuwa huu ni mwendelezo wa Kampeni yao itakayodumu kwa takribani miaka miwili tangu walipoanza na lengo likiwa nikuwafanya wanafunzi hususani wa darasa la saba wawe na ufahamu zaidi juu ya chanzo kingine cha umeme ambacho ni rafiki wa mazingira kwa kupitia mafunzo katika madarasa yao katika hafla fupi iliyofanyika ofisini kwa Mh. Edward Lowassa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya DoulbeTree by Hilton Florenso Kirambata.
IMG_9437
Mkurugenzi wa Kanda wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton ya Dar es Salaam Bw. Judd Lehmann (katikati) akimkabidhi moja kati ya taa 200 zinazotumia nishati ya jua Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli Mh. Edward Lowassa. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya DoulbeTree by Hilton Florenso Kirambata akishuhudia tukio hilo kwenye hafla fupi iliyofanyika Ofisini kwa Mh. Edward Lowassa jijini Dar.
IMG_9448
Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya DoulbeTree by Hilton Florenso Kirambata akikabidhi baadhi ya taa zinazotumia nishati ya jua kwa Kaimu Afisa Elimu wa Wilaya ya Monduli Jumanne Masuke. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Waziri Mkuu wa zamani Mh. Edward Lowassa ( wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Kanda wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton ya Dar es Salaam Bw. Judd Lehmann (wa pili kushoto).
IMG_9468
Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli Mh. Edward Lowassa akitoa shukrani kwa uongozi wa DoubleTree Foundation ambapo ametumia fursa hiyo kuitaka serikali kuwekeza sana katika elimu ili kuweza kukuza uchumi.
Aidha amesema ni vyema kuwekeza katika sekta ya elimu ili tuweze kusonga mbele na kuwa na kizazi cha watu wenye elimu kwani masikini asiye na elimu ni hatari kuliko mtu yeyote, kwa kuwa mtu anapopata elimu anakuwa na ufahamu unaomuwezesha kukabiliana na maisha ya kila siku.
IMG_9481
Picha juu na chini ni Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli Mh. Edward Lowassa akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Kanda wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton ya Dar es Salaam Bw. Judd Lehmann (katikati) na Kushoto ni Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya DoulbeTree by Hilton Florenso Kirambata mara baada ya kukabidhiwa taa 200 zinazotumia nishati ya jua atakazozigawa katika jimbo lake kwa shule za msingi.
IMG_9479

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post