Waziri Mkuu Pinda
kukabidhi Madawa yenye Thamani yatsh.16.2 milion kwa Hospitali ya mkoa mount Meru wakati atakapowatembelea
wagonjwa walipata majeruhi kwenye muendelezo uliotokea jana wa mlipuko wa bomu kwenye Kanisa la Mtakatifu
Joseph Mfanyakazi eneo La olasiti Nje
kidogo ya Jiji la Arusha.
Akizungumza
wakati akitoa Mablanketi kwa niaba ya wizara ya utalii kupitia shirika la
hifadhi la taifa (TANAPA)Naibu waziri wa Maliasili na utalii Lazaro Nyalandu
alisema kuwa wizara yake kupitia Tanapa wametoa vifaa hivyo ili kusaidia
hospitali hiyo yenye uhuba wa madawa na vifaa mbali mbali ikiwemo upungufu wa
vitanda,madawa na mablanketi ambayo sehemu ya madawa itakabidhiwa jioni na Mh.waziri
mkuu kwa niaba ya serekali.
“Kwanza
tunatoa pole kwa majeruhi wote waliopatwa na tukio hilo na tunawatakia wapone
haraka pili msaada huu tunautoa kwa ajili ya kupunguza upungufu uliotokea
kwenye hospitali yetu ntakaa na wenzangu wadau wa utalii tuangalie nini cha
kufanya” alisema nyalandu.
Alisema kuwa
jumla ya tsh.16.2 milion zitatumika kununulia madawa ambayo ya takabidhiwa
jioni na waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mizengo Peter Pinda.
Wakati huo
huo kijana wa miaka 16 mkazi wa Olasiti James Gerald amefariki dunia usiku wa
kuamkia Leo ikiwa ni mtu wa pili kufariki katika tukio la mlipuko wa bomu
uliotokea kwenye kanisa la Joseph Mfanyakazi kwenye kata ya Olasit jijini
Arusha.
Akithibitisha
kutokea kwa mauti hayo Kaimu mganga mkuu wa Hospitali ya Mount Meru dkt.Mariam
Murtazah alisema kuwa hospitali hiyo ilibidi kuongeza dawa kutokana na wingi wa
watu na kuwa msaada waliupata umekuja wakati muafaka kwani hospitali hiyo
inakabiliwa na upungufu wa vifaa yakiwemo madawa.
Aidha Askofu
mkuu wa JImbo kuu la katoliki Arusha Josephat Lebulu Akiongozana na Balozi wa Vatikan
hapa nchini Fransisco Padilla waliwatembelea majeruhi wa mlipuko wa mabomu
majra ya saa 11;39 na kuwafariji majeruhi hao kwa kuwawekea mkono wa Baraka kwenye
mapaji ya uso.
Akizungumza
na waandishi wa habari baada ya kutoka kuwatembelea majeruhi hao alisema
wamepata salamu mbali mbali kutoka mataifa mbali mbali wakiwatakia majeruhi hao
wapone haraka na rambi rambi kwa wafiwa huku akitoa tamko la kanisa kuwa ni
mafundisho ya bwana yesu kuwa tuushinde ubaya.
Lebulu
aliwataka wakirsto hapa watanzania kuweka ulinzi wao moyoni badala ya kutegemea
polisi kwani majaribu ya shetani ni mengi kama unavyoona shetani anatumia watu
kupiga mabomu hadi kwenye nyumba za ibada,hata ukiweka ulinzi kwenye nyumba za
ibada bado shetani ataendelea kuwatumia wafuasi wake.
“Tuweke
ulinzi rohoni mwetu kwanza kabla ya kuuweka mbele ulinzi wa Askari wetu hakika
kama hatutatumika na shetani basi matukio kama haya yatakuwa historia”alisema
Lebulu mbele ya balozi Padilla
Mahmoud
Ahmad Arusha