Gari la maji yakuwasha lahishiwa halina maji, askari walipanda wakashuka kulikimbia
WATU watatu wamefariki Dunia katika mapambano ya Askari Polisi na
Wananchi waliokuwa wakiandamana kupinga hotuba ya Bajeti ya Wizara ya
Nishati na Madini iliyosomwa leo na Waziri Profesa Sospeter Muhongo.
Mbali na watu hao kuuawa Askari mmoja wa Jeshi la Polisi pia
amejeruhiwa vibaya baada ya kuchomwa mshare katika mapambano hayo
yaliyoanza saa 12 asubuhi,katika maaeneo mbalimbali yaliyokuwa yametekwa
na waandamanaji hao.
Mwandishi wa Habarimpya.com aliyekuwa katika maeneo
ya Mikindani anaripoti kwamba watu hao waliuawa katika eneo hilo baada
ya kutokea kwa mapambano makali kati ya waandamanaji na Askari Polisi.
Mbali na mauaji hayo pia kumetokea uharibifu mkubwa wa mali katika eneo hilo ambapo ofisi
za serikali zimevamiwa na kuchomwa moto huku daraja la Mikindani nalo
likivamiwa na kuvunjwa ili kuzuia mawasiliano pamoja mwingiliano wa watu
kutoka Mtwara mjini kuingia eneo hilo.
"Mapambano ni makali katika eneo la Shangani huku waandamanaji
hao wakielekea kwenye nyumba za vigogo zilizopo jirani na eneo mapigano
kwa sasa, hivi tunavyozungumza tumehifadhiwa katika Kanisa moja hapa
maeneo ya sokoni, na kuna nyumba moja ya kulala wageni (Shengena Lodge)
pia imechomwa moto kwa madai kwamba iliwalaza Askari Polisi walioingia
hapa Mtwara tangu juzi kwa ajili ya kuthibiti machafuko, hali ni mbaya
milio ya risasi na mabomu ndiyo yanayosikika"alisema Mwandishi wa Habarimpya.com.