Lema hospitaliniMbunge
wa Arusha mjini Godbless Lema akiwa na mbunge wa Arumeru Joshua Nassari
wametoa damu kwa ajili ya majeruhi walioumia katika mlipuko huo.
Lema
amewahimiza wakazi wa Arusha na vijana kujitolea kwa wingi kuchangia
damu ili kuokoa maisha ya majeruhi. Watu wengi wameitikia wito na
wanaendelea kujitolea kuchangia damu kama ishara ya kumuunga mkono
mbunge wao.
Ulinzi umeimarishwa
Viongozi
wa Kanisa wakitoa taarifa ya kilichotokea kwa waandishi wa habari kabla
ya Balozi wa Papa kuondolewa Kanisani hapo chini ya ulinzi mkali wa
Polisi.
Meya
wa Manispaa ya Arusha, Mh gaundence Lyimo akielekea eneo la tukio kwa
miguu baada ya utaratibu wa kutumia magari kuwa mgumu kutokana na idadi
kubwa ya watu na magari yaliyoziba njia.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, magesa Mulongo akijiandaa kuzungumza na wananchi
kanisani hapo na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha watu wote
waliohusika na jaribio hilo ovu, pamoja na mtandao wao wanakamatwa.
Alidai pia vikosi vya Jeshi maalumu kwa kuchunguza milipuko vitafika
eneo hilo ili kufanya uchunguzi. Taarifa za eneo la tukio zinaeleza kuwa
tayari kuna mshukiwa mmoja ameshatiwa mbaroni na yuko mikononi mwa
Jeshi la Polisi kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.
Eneo
lenye utepe ndipo kitu hicho kinachodhaniwa kuwa bomu kilipoangukia.
Pichani unaweza kuona wigi za kichwani na viatu vya waumini vikiwa
vimesambaa baada ya wenyewe kuviacha, miongoni mwao wakiwa ni majeruhi.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo akizungumza na mmoja wa mapadri wa
Kanisa hilo kupewa maelezo ya kuhusu kilichotokea kanisani hapo.