Na Mwandishi Wetu
Kituo kikuu cha mabasi cha wilaya ya Hai
kilichopo katika mji wa Bomang'ombe kimefungwa kwa muda ili kupisha
matengenezo makubwa ya kuweka lami.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus
Makunga amewaeleza waandishi wa habari kwamba matengenezo hayo
yanayokana na ahadi ya rais Jakaya Kikwete wakati wa kampeni za uchaguzi
wa mwaka 2010.
Ameeleza kuwa matengenezo hayo ya kipande cha urefu wa kilometa 0.85 utachukuwa siku 45 kwa gharama ya shilingi milioni 90.
Amefafanua
kwamba matengenezo hayo yataunganisha barabara inayoingia kituoni hapo
na ile ya Moshi hadi Arusha pamoja na kukiwekea lami.
Makunga ameeleza kuwa wakati kituo hicho kikiwa kimefungwa,hivi sasa kinatumika kituo cha muda katika eneo la Double road
Ameeleza
kuwa katika mwaka wa fedha wa 2012/2013,Halmashauri ya wilaya ya Hai
ilitengewa jumla ya shilingi 460,810,000 katika mfuko wa barabara.
Wilaya
ya Hai ina barabara zenye urefu wa kilometa 466.2 ambapo kati ya
hizo,kilomeya 32 ni barabara kuu,kilometa 42 ni za mkoa,kilometa 175.93
ni za wilaya na kilometa 150.27 ni za vijiji na barabara za Hai ni
kilometa 66.
Amesema kuwa barabara zinazopitika nyakati zote ni kilometa 235.53 ambazo ni sawa na asilimia 50.82
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia