Jeshi la
polisi mkoani hapa limefanikiwa kukamata magunia 30 ya bangi huku askari wawili
wa jeshi hilo mkoani hapa wakikamatwa wakati wakisindikiza magunia 18 ya madawa
ya kulevya aina ya mirungi kwenye mpaka wa nchi na Kenya Holili mkoani
Kilimanjaro.
Akizungumza
na vyombo vya habari Kamanda wa jeshi hilo mkoani hapa kamishna wa msaidizi wa
polisi Liberatus Sabas alisema kuwa mnamo tarehe 19 mwezi huu huko mpakani mwa
nchi ya Kenya na Tanzania Holili mkoani Kilimanjaro askari wawili wa Jeshi hilo
mkoani hapa Koplo Edward na Mwenzake pc.George walikimatwa akisindikiza mirungi
magunia kumi nane.
Kamanda
Sabas alisema kuwa watuhumiwa hao wapo mkoani Kilimanjaro na taarifa zao anazo
kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz alibainisha kuwa jeshi hilo
limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu wakiwa na bangi magunia 30 katika
msako mkali walioufanya kwenye kata ya Ngarenanyuki wilayani Meru.
Sabas
alibainisha kuwa wengine wawili walikimbia na jeshi hilo linawatafuta katika
hatua nyingine jeshi hilo limakamata gari lenye namba za usajili KBQ372V
lililoibiwa nchi jirani ya Kenya majira ya saa 6:30 usiku huko wilayani Longido.
Kamanda
Sabas alisema kuwa katika kupambana na mitandao ya madawa ya kulevya
walifanikiwa kuwakamata askari hao na kuwataka watanzania na wakazi wa mkoa huu
kutoa taarifa zitazosaidia kumaliza matukio ya kiuhalifu mkoani Arusha kwani
Arusha bila ya madawa ya kulevya inawezekana na nchi vile vile pia
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia