Baadhi ya washiriki wa Redds Miss Manyara 2013,wakifanya mazoezi ya
kujiandaa na mchuano wa kumtafuta mnyange wa mkoa huo utakaofanyika
mjini Babati Juni mosi mwaka huu
Jahazi morden tarabu ikiwa chini wa muimbaji mashuhuri Mzee Yusuphyinatarajia kuinogesha usiku wa kumsaka mlimbwende wa mkoa wa Arusha
(Redds Miss Arusha) inatarajiwa kufanyika June nane mwaka huu katika
ukumbi wa triple A uliopo jijini apa.
Akizungumza na waandishi wa habari muandaaji wa shindano hilo Phidesia
Mwakatalima alisema kuwa shindano hilo litafanyika usiku wa jumamosi
june nane katika uwanja wa ukumbi wa Triple A uliopo ndani ya jiji la
Arusha.
Alisema kuwa jumla ya walibwende kumi na tano 15 kutoka katika
vitongoji vitatu vya jiji la Arusha ambapo alivitaja kuwa ni pamoja na
kitongoji cha Njiro,Arusha mjini(Arusha city cetre)pamoja na kitongoji
cha Monduli.
Alibainisha kuwa mpaka sasa warembo wameshaingia kambini wameanza
kujifua kwa ajili ya shindano hilo huku akibainisha kuwa kwa mwaka huu
lazima mrembo wa Tanzania (Redds Miss Tanzania )atokee mkoa wa Arusha
Alisema kuwa zawadi mbalimbali zitatolewa ikiwemo kuwasomesha warembo
katika vyuo mbalimbali lungha ya kiswahili ,kingereza pamoja na
kifaransa.
kwa upande wa wathamini waliothamini shindano hili walisema kuwa ni
pamoja na perfect choice super markety,libeneke la kaskazini
blog,trile A fm,Radio 5 fm,sunrise Fm,Mambo Jambo Fm,Alayance
france,Geo Securty,Cassaranda wear,Meru Spring Water Pamoja na Otakef
Motel.