Katibu
mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Techinojia Dkt. Forens Turuka
(katikati) akisisitiza jamboa baada ya kumkabithi kitabu cha Majukumu na
Mafanikio ya Wizara hiyo toka kuanzishwa kwake mpaka mwaka 2011,
Mwenyekiti wa Taifa wa Tughe Dkt. Diwani Mruttu(wa pili kulia).Kushoto
ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Raslimali watu Bi Mazoea Mwera
kwenye Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi ulifanyika mwishoni wa wiki
jijini Dare s Salaam.
Katibu
mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Techinojia Dkt. Forens Turuka
(kushoto) akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi
wa wizara hiyo mwishoni mwa wiki. Mwenyekiti wa Taifa wa Tughe Dkt.
Diwani Mruttu ( wapili kulia), Watatu kulia kulia ni Mkurugenzi Msaidizi
wa Utawala na Utumishi , Bi. Mazoea Mwera.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Wizara
ya Mawasiliano,Sayansi na Techinolojia imesema imeweza kutekeleza
majukumu yake makubwa kwa ufanisi mkubwa katika mwaka wa fedha uliopita
hivyo kuwapongeza wadau na wafanyakazi wake kwa kufikia malengo.
Waziri
wa Mawasiliano,Sayansi na Technolojia Pof.Makame Mbarawa amewapongeza
wafanyakazi wa Wizara hiyo kwa kazi nzuri waliyoifanya kupita Mkutano wa
Baraza la wafanyakazi la Wizara hiyo .
“Suala
la bajeti ndogo halikuwa kikwazo kwa wafanyakazi kutekeleza majukumu
yao na akawataka kuendelea na moyo huo wa kutumia rasilimali kidogo
zilizopo kwa ufanisi mkubwa,” alisema Prof.Mbarawa katika hotoba yake
iliyomwa na Katibu Mkuu katika Wizara hiyo Dk. Florens Turuka kwenye
Baraza la Wafanyakazi mwishoni mwa wiki.
Amesema
vizara imeweza kutekeleza kwa mafanikio makubwa malengo iliyojiwekea
pamoja na kuwepo kwa changamoto zilizojitokeza na kusema maeneo ambayo
yalileta changamoto katika utekelezaji wake kuwa yatafanyiwa kazi katika
mwaka wa fedha unaoanza. Amesema baraza ndio chombo cha uwakilishi wa
wafanyakazi wa Wizara kwahiyo chochote kikienda hovyo katika utekelezaji
wa majukumu ya Wizara baraza la wafanyakazi ndilo litawajibika kujibu
maswali toka kwa menejimenti.
Amewataka
wafanyakazi kuwa na moyo wa kujituma na akasisitiza kuwa kupitia kauli
mbiu ya “kwa dhamira ya kweli,uwajibikaji wa kweli,yote yanawezekana”
mengi yameweza kufanyika.
Ameyataja
baadhi ya maeneo ambayo wizara inajivunia kuyatekeleza kwa ufanisi kuwa
ni eneo la kufungwa kwa mkongo wa taifa ambao umepunguza gharama za
kuunganisha simu tioka mtandao mmoja kwenda mwingine hivyo kuwapunguzia
wateja mzigo wa kutembea na simu zaidi ya tatu.
Eneo
lingine ni kuanzishwa kwa timu maalum ya kudhibiti mawasiliano kwenye
komputa ili kudhibiti watu wenye nia mbaya ambao wanaingilia mitandao ya
wenzao na kufanya mambo yasio na heshima kwa jamii.
Ametaja
kuanzishwa kwa Taasisi ya Techolojia ya Nelson Mandela ambacho ni moja
kati ya Chuo bora katika afrika chenye mlengo wa kuibua wanasayansi bora
ambao wataweza kubadili sura ya taifa kimaendeleo kutokana na elimu
waliyoipata.Suala la utambuzi wa makazi pamoja na anuani za makazi hayo
nalo limetajwa kuendelea vizuri.
Wakati
huo huo,Mwenyekiti wa Tughe Taifa Dkt Diwani Mruttu amewataka
wafanyakzai wa wizara hiyo kuendelea na moyo wa kujituma kufwatia unyeti
wa sekta wanaoiongoza.
Amesema
watu wengi hawaoni umuhimu wa wizara hiyo ila siku simu zote zikizima
kwa mda wa saa moja ndipo watu wanaweza kuona umuhimu wa wizara
hiyo.”Kama simu zingezimwa siku ya mgomo wa madaktari mwaka jana ata
mgomo usingekuwepo……,tungeratibu vipi mgomo huo bila
mawasiliano?”alihoji.
Amewataka
wafanyakazi kuwa na utamaduni wa kujifanyia tahthimini ya kile
wanachokifanya ili kuweza kugundua mapunguafu na kuchukua hatua haraka.
Amewaasa
wafanyakazi kuwa na utamaduni wa kupima afya zao na wasingoje mpaka
wajisikie kuumwa ndio waendendee hospitali kwani kufanya hivyo
kutosimamisha kazi za wizara hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya wizara
hiyo.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia