pole mtoto mungu atakusaidia utapona maneno haya makamu wa rais alimwambia mtoto huyu wakati alipotembelea majeruhi katika hospitali ya mounti meru
mbunge wa jimbo la Arusha mjini katika kati Godbless Lema akiwa na mbunge wa jimbo la Arumeru mashariki Joshua Nassari wakiangalia kanisa ambalo limelipuliwa na bomu hivi leo asubui
Baadhi ya wananchi wakiwa wanafurahia mara baada ya kuvunja geti la hospitali ya mkoa ambapo awali mlinzi alidai kuwa funguo umepotea huku gari ya majeruhi ikiwa inasubiri kufunguliwa geti ili ipitishe mgonjwa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr,Mohame Bilal akiwa anawapa pole majeruhi waliolazwa katika hospitali ya mkoa ya Mounti Meru mara baada ya kulipukiwa na bomu wakati wakiwa katika misa ya uzinduzi wakanisa la Mt,Josephy Mfanyakazi katika kata ya Olasiti jijini Arusha
MTU mmoja
amekamatwa na anaendelea kuhojiwa na polisi kufuatia mlipuko mkubwa wa bomu
lililorushwa kwa waumini wa Kanisa Katoliki jana ambapo watu 66 wamejeruhiwa
wakiwamo wanawake 41 na wanaume 25, huku majeruhi wawili hali zao zikiwa mbaya
zaidi.
Mkuu
wa Mkoa
wa Arusha, Magesa Mulongo alimweleza Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib
Bilal
na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema,naibu waziri wa mambo ya
ndani PereiSilima,na naibu waziri wa nishati na madini Stephen Masele
wakati walipowatembelea majeruhi
waliolazwa katika Hospitali ya Mount Meru jana jioni.
Alisema kati
ya majeruhi hao wawili hali zao ni mbaya, huku mmoja akiwa akiwa amepelekwa
hospitali ya KCMC kwa matibabu zaidi.
Makamu wa
Rais alitarajiwa kuondoka na majeruhi mwingine mtoto ambaye anapelekwa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Mulongo alithibitisha
kwamba aliyefariki katika tukio hilo ni mama mmoja ambaye wa kwanya ya Kimasai
ambayo ilikuwa ikiimba kwenye shughuli za uzinduzi wa kanisa hilo.
Akitoa pole
kwa wagonjwa waliolazwa pia kwa wale ambao jamaa zao wamepata maradhara kwa
tukio hilo, kwa waumini wa Kanisa Katoliki, kwa wakazi wa Arusha na Watanzania
kwa ujumla, Dk Bilal alisema tukio hilo ni la aibu na baya sana.
“Tukio hili
ni la aibu sana, baya, limeshtusha kutokea hapa nchini, serikali inalaani na
itafanya kila linalowezekana kuwatia mbaroni wahusika na tayari imekwishaanza
kuhakikisha wahusika wanakamatwa.
“Vyombo vya
usalama vimeagizwa kufanya kazi hii usiku na mchana kuhakikisha kwamba wahusika
wanakamatwa na wanachukuliwa hatua,” alisema.
Mkuu wa
Jeshi la Polisi, Mwema akitokea Dodoma kuhudhuria vikao vya bunge ambako leo
Wizara ya Mambo ya Ndani inawasilisha bajeti yake, alielezea tukio hilo kuwa ni
la kushutua sana.
“Ni tukio la
kushtua, kusikitisha, tumefika eneo la tukio na mpaka sasa mtu mmoja amekamatwa
na anaonyesha ushirikiano mzuri wa kutoa taarifa.
“Tukio kama
hili sio la mtu mmoja, wapo waliohusika katika kupanga, kuratibu, kushauri,
kuchangia gharama na wale waliofanikisha. Hata huyu mmoja aliyekamatwa ni
mchango wa ushirikiano wenu, naombeni muendelee kushirikiana na polisi katika
kufanikisha uchunguzi huu.
Kwa upande
wake, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malasusa, ambaye
aliambatana na Makamu wa Rais kutokea mkoani Shinyanga, alisema amesikitishwa
sana na tukio hilo.
Alisema tukio
hilo sio la kawaida na limewashtua watu wengi wanaopenda amani lakini amewaomba
waendelee kuwa watulivu wakati suala hili linapoendelea kufanyiwa uchunguzi.
“Wakristo
tuendelee kuhubiri amani, kuombea amani kwa sababu Mungu wetu ni wa amani,”
alisema.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia