Kijana Sydney Wilhelm Gidabuday mmarekani mwenye asili ya kitanzania na
mtoto wa mwanaharakati wa mchezo wa riadha nchini Tanzania "Wilhelm
Gidabuday" anaendelea kufuata nyayo za baba yake baada ya kutwaa ushindi
katika mashindano ya riadha yaliyofanyika huko California nchini
marekani.
SYDNEY WILHELM GIDABUDAY |
Sydney Gidabuday anayetimiza miaka 18 mwakani akiwa ni raia wa marekani
huko California, anazidi kukamata tuzo mbali mbali za mashindano ya
riadha huko California, ambapo mwaka 1994 baba yake ambae ni mtanzania
na mzalendo wa mchezo wa riadha alishikilia ubingwa wa riadha huko
California Marekani.
SYDNEY WILHELM GIDABUDAY - akiongoza mashindano ya riadha ya 32OOM CIF CHAMPIONSHIPS; huko California Marekani |