ALBERT MANGWEA AKIWAJIBIKA ENZI ZA UHAI WAKE KWA MASHABIKI WAKE.MWILI WA MAREHEM ALBERT MANGWEA AFRIKA YA KUSINI.
DAR ES SALAAM.
WAKATI mazishi ya mwanamuziki marehemu Albert Mangwea(28) maarufu kama `Ngwair’ yakitarajiwa kufanyika mjini Morogoro, maeneo ya Kihonda baada ya mwili kuwasili nchini, hospitali iliyomfanyia vipimo imethibitisha kuwa pombe na dawa za kulevya kupita kiasi ndivyo vilivyomuua.
WAKATI mazishi ya mwanamuziki marehemu Albert Mangwea(28) maarufu kama `Ngwair’ yakitarajiwa kufanyika mjini Morogoro, maeneo ya Kihonda baada ya mwili kuwasili nchini, hospitali iliyomfanyia vipimo imethibitisha kuwa pombe na dawa za kulevya kupita kiasi ndivyo vilivyomuua.
Mwili wa mwanamuziki huyo, ambaye alitamba kwenye
miaka ya 2000 na wimbo wa `Mikasi’, unatazamiwa kuletwa kesho nchini na
kuagwa Jumamosi kabla ya kusafirishwa kwenda kwao Kihonda, Morogoro kwa
mazishi.
Kwa mujibu wa taarifa Mangwea alifariki dunia juzi
kwenye Hospitali ya St Hellen, iliyopo Johannesburg, Afrika Kusini
alikokuwa amekwenda kwa shughuli za muziki.
Kifo chake
Ripoti iliyochapwa na mitandao mbalimbali ya ndani
na nje ya nchi inasema marehemu alifikwa na umauti baada ya kulewa
kupindukia, kibaya zaidi alikuwa hajala.
Siku ya kifo chake, Mangwea alianguka nyumbani kwa rafiki zake akiwa katika hali hiyo ya kulewa sana.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, baada ya kufikishwa
hospitalini, Mangwea aligundulika kulewa mara tano ya kipimo cha kilevi
kilichopitishwa na serikali ya Afrika ya Kusini, ambacho ni 416mg za
pombe kwenye kila milimita 100(kwa mlevi anayeendesha chombo cha moto).
Pia marehemu alikutwa na upungufu wa hewa ya oksijeni kwenye seli na tishu za mwili wake.
Ripoti hiyo ilibainisha kuwa Mangwea, maarufu
Ngwair, alikuwa na tatizo la kutokula chakula vizuri kabla ya kifo chake
na pia kukosa muda wa kupumzika.
Sampuli zilizopatikana mwilini mwake zinaonyesha
mkusanyiko wa dawa za kulevya mbalimbali zikiwemo heroine, cocaine chafu
na bangi ya gramu 0.08 ambavyo vilikutwa kwenye damu yake.
Kifo chake kilitokana na mshtuko wa moyo na
kushindwa kupumua, hali iliyosababisha mapigo ya moyo wake kusimama kwa
sekunde chache, na kusababisha kifo chake.
Mwili wa Ngwair ulionekana kana kwamba alitokwa na
damu nyingi puani baada ya kuonyeshwa kwa Watanzania wengi jana jioni
Johannesburg, Afrika Kusini.