Timu
ya Tanzania ya kuogelea ikiwa katika picha ya pamoja baada ya kupewa
kikombe cha mshindi wa Tatu jumla kwa kupata alama 230.
Timu ya vijana kutoka Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na makocha wao wakiwa nyuma.
Nahodha
wa Timu ya Taifa ya kuogelea,Sonia Tumioto (katikati) akiwa na bendera
ya Tanzania baada ya kupokea zawadi ya kikombe cha mshindi wa kwanza kwa
wanawake.
Timu
ya vijana ya kuogelea kutoka Tanzania imefanya vizuri katika mashindano
yaliyoshirikisha timu 20 kutoka ukanda huu wa Afrika Mashariki na
mashindano hayo kufanyika jijini Nairobi kuanzia tarehe 17 hadi 19 May
2013 katika shule ya Aga Khan. Washiriki wa mashindano hayo walitoka
katika nchi za Tanzania, Kenya, na Uganda ambazo kila mmoja alitaka
kumshinda mwenzake.
Wasichana
kutoka Tanzania wamekuwa washindi wa kwanza kwa kupata alama176 points
dhidi ya timu 24. Timu ya Uganda Dolphins imeshika nafasi ya pili kwa
kupata alama 148 ambao walijaribu kuonyesha upinzani kwa timu yetu. Timu
ya Tanzania kwa upande wa wanaume imeshika nafasi ya 6 dhidi ya timu za
wanaume 19 zilizoshiriki katika mashindano hayo.
Hii
ilisababishwa na ukweli hatukwenda na wachezaji wa kutosha kiasi
hawakuweza kushiriki katika relay na tulipata alama 54. Matokeo ya jumla
ni kuwa Tanzania tumekuwa watatu kwa kupata alama 230 ambapo Dolphins
Uganda wamekuwa wa kwanza kwa kupata alama 278 na Makini ya Kenya wapili
kwa kupata alama 240.50.
Waogeleaji
wetu walikuwa na ari ya juu licha ya hofu tulikuwa nayo hapo kabla ya
baridi kali na tunamshukuru Mwenyezi Mungu hakukuwa na baridi kali labda
wakati wa usiku. Muda wote wa mashindano waogeleaji wetu wakati
wanapiga mbizi walishangiliwa kwa sauti ya juu na shukrani kwa wazazi
ambao muda wote walikuwa wanashangilia ``Tanzania oye``.
Kwa
hakika ni matokeo ya kufurahisha licha ya medali, wachezaji wetu
waliweza kushusha muda wao na kuweka muda mpya(PB)na wengine
wameteremsha muda wao hadi sekunde 10. Waogeleaji wetu walikuwa walikuwa
katika kiwango bora kuanzia siku ya mwanzo ya mashindano walipoanza
kuogelea mita 100 (IM) muogeleaji anaogelea stroke zote 4. (25m
butterfly, 25m backstroke, 25m breastroke and 25m freestyle).
Kila
aliyeshiriki alikuwa anajaribu kumshinda mpinzani wake na kwa kweli
tulikuwa na ushindani mkali kutoka kwa waganda na wakenya . Muogeleaji
Sonia Tumiotto (KAPTENI WA TIMU) alipata dhahabu na kuweka rekodi ya
mashindano kwa wasichana miaka 11 mita 100 IM kwa kuogelea muda mpya wa
dakika 1:18:70. Medali ya silver ilienda kwa Smriti Gokarn ambaye
alikuwa na upinzani mkali kutoka kwa wasichana wenzake miaka 10 na
kuogelea muda wa dakika 1.25.54 Siku ya pili ya mashindano hayo waogeaji
wetu waliweza kupata mbalimbali wakiwemo. Selina Itatiro (silver, miaka
9 wasichana, 25m fly), Tessa Francis (bronze, miaka 9 wasichana 25m
fly, na silver 25m free), Smriti Gokarn (silver, 50m fly. Silver 50m
breast, dhahabu 50m back, silver 25 free), Sonia Tumiotto(11) (Dhahabu,
50m fly, dhahabu 50m breast, dhahabu 50 back, dhahabu 25 free), Amani
Doggart (bronze miaka 8 wasichana 25m breast) ,Njukia kihara (silver,
miaka 7 breast), Dhashraad Magevaran (10)(bronze, 50m back).
Waogeleaji
wetu pia wamekuwa washindi na kupewa zawadi ya vikombe kwa kila umri.
Waliopata vikombe kwa wasichana miaka 8 ni Amani Doggart nafasi ya tatu,
Tessa Francis miaka 9 wasichana nafasi ya tatu, Smriti Gokarn miaka 10
nafasi ya pili na kuweka rekodi mbili na Sonia Tumiotto miaka 11
wasichana nafasi ya kwanza na kuweka rekodi 3.
Siku
ya jumapili ilikuwa ndio siku muhimu na ya kweli kwa Tanzania ambapo
waogeleaji wa relay waliweza kupata dhahabu kila tukio tuliloshiriki.
Katika miaka 8 wasichana kwa timu ya relay iliyowashirikisha Diya Patel,
Maia Tumiotto, Ursula Khimji and Amani Doggart walipata dhahabu mbili
kwa medley relay(KILA MUOGELEAJI ANAOGELEA AINA MOJA YA MTINDO WA
KUOGELEA) na freestyle relays, wasishana wa miaka 11 yenye waogeleaji
Sonia Tumioto, Selina Mehta, Maya Kihara, Tallin Stengell nao waliweza
kuchukua medali mbili za dhahabu kwa medley relay na freestyle relays.
Miaka 10 wavulana kwa tim u yenye waogeleaji Dhashraad Magesvaran, Urav
Shah, Alexander Belikov and Vansh Ladwa nao walichukua dhahabu katika
mtindo wa medley relay and freestlye relays. Juhudi za pamoja kati ya
wasichana na wavulana ndizo zilizotuwezesha Tanzania kuwa nafasi ya tatu
kwa matokeo ya jumla kwa mwaka 2013 Naye kocha wa timu hiyo Mohamed
Abdulazizi alisema kuwa “Tuliwaandaa wachezaji kimwili na kiakili kuweza
kukabiliana na lolote litakalojitokeza mbele yetu ndio siri ya
mafanikio haya ya kufurahisha.
Tanzania
iliwakilishwa na Sonia Tumiotto (Team captain), Harry McIntosh (vice
captain), Dashraad Magesvaran (boys captain), Smriti Gokarn (girls
captain), Reuben Monyo, Njukia Kihara, Prashraad Magesvaran, Oliver
McIntosh, Shiv Shreekumar, Gian Maria, Vansh Ladwa, Alexander Belikov,
Urav Shah, Maia Tumiotto, Diya Patel, Amani Doggart, Celina Itatiro,
Tessa Francis, Janice Njuguna, Selina Mehta, Maya Kihara, Mariana
Pipollo, Piya Shah, Talin Stengel and Ursula Khimji.
Makocha
wengine wqa timu hiyo ya waogeleaji 25 walikuwa ni Kocha Alex Mwaipasi
na Kocha Kanis Mabena na Mkuu wa msafara alikuwa ni Inviolata Rwelamira
Itatiro.
Tunajivunia
vijana hawa kwa kutuwakilisha vyema na kufanya Tanzania kungára,
Hongera sana pamoja na wazazi wote. Hii ni mara ya pili katika historia
ya mchezo wa kuogelea ambapo timu ya vijana imeweza kwenda kushiriki
mashindano ya Afrika Mashariki na kurudi na vikombe na medali nyingi.
Mara ya kwanza ilikuwa timu ya vijana pia ilipoweza kurudi kwa kikombe
cha mshindi wa pili baada ya kujikusanyia medali 76 ambapo mashindano
hayo yalifanyika Kampala mwezi wa 10 tarehe 22 na 23 mwaka 2011.
RAMADHAN NAMKOVEKA
ASSISTANT GENERAL SECRETARY
TANZANIA SWIMMING ASSOCIATION (TSA)