BREAKING NEWS

Wednesday, May 29, 2013

MSANII NGWEA AFARIKI DUNIA NCHINI AFRIKA KUSINI


MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Albert Mangwea 'Ngwea'au mimi au Cowboy amefariki dunia Afrika Kusini leo.
Taarifa zilizopatikana leo kutoka Afrika Kusini ambapo inasemekana msanii huyo alikuwa akiishi, zinasema Ngwea alifikwa na umauti mapema leo.

Habari toka afrika kusini zinasema kuwa Ngwea a.k.a mimi, Coboy alifikwa na umauti kwenye hospitali ya  St Hellen mjini hapo Johanesbaerg alikokuwa amelazwa.

Hata hivyo, haijajulikana mara moja sababu ya kifo cha Mangwea ambaye alikuwa mmoja wa wasanii kutoka  chamber squad 'East Zoo'.

Mangwea alianza kujulikana kwenye ulimwengu wa muziki mwanzoni mwa miaka ya 2000 na nyimbo zake zilizomtambulisha vilivyo na kujizolea mashabiki wa muziki ni Mikasi na  Gheto Langu.
Ngwea ameshirikiana na wasanii kaza wa Muziki wa Kizazi kipya hapa nchini kama AY, TID, Mchizi Mox, Ferouz, Raha P na wengine kibao.


BAADHI YA NYIMBO ZA NGWAIR NI HIZI
Verse:- I Ngwea
Ni asubuhi naamka ninapiga mswaki
Kisha naenda kubath kuweka mwili safi
Narudi ghetto nafungua kabati
Nachukua pamba blingbling kwa chati
Nna t-shirt black nna jeanz ya kaki
Na chini nina simple white chata nike
Kisha mzee najipulizia marashi
Nanukia safi
Niko na machizi wa chamber squad na Dark
Tunawapigia simu Rich Coast wako wapi
Tunakutana mitaa ya Chaga Bite
Asubuhi tunapata zetu supu kwa chapati
Na mitungi ya kupotezea wakati
Ukitaka fegi mezani kuna pakti
Iwe sm yani sports au embassy
Hapa utakula raha mpaka mwenyewe utasema basi
Tunakamua mpaka ile mida ya lunch
Tunaagiza ugali mkubwa na samaki
Makamuzi yanaendelea mpaka night
Watu wanaingia graveyard kwanza kupata nyasi
Tunarudi kila mmoja anajisachi
Ni kiasi gani mfukoni kilichobaki
Kujicheki mi nna kama laki
Nikawaambia machizi kinachofuata MIKASI

Kiitikio:- Ferouz
Mitungi,blunt mikasi{oooh yeeeaaaaaaaah}
Kama ukitaka kuvinjari nasi basi
Mfukoni mwako nawe uwe safi
rudia kiitikio x2

Verse:- II Ngwea
Kulewa tushalewa kilichobaki mikasi
Washikaji eh milupo tutapata wapi?
Milupo labda mitaa ya kati
so tunaenda vipi kwa miguu au kwa basi?
Usiku huu bora tuchukue tax
Poa basi tusiponaita tax
Njo utupeleke mitaa ya kati
Tukacheki midudu ya kupiga mikasi
Tuelewane kabisa itatucost sh’ngapi?
{4000 tu}
Aah wapi
Kwani hapa na pale ni umabali wa hatua ngapi?
{Si unacheki mwenyewe mko wangapi}
Usimind sana babake hatuko safi
Tuchangeni tusipoteze wakati
Ludigo kwani we una tshs ngapi?{buku tano}
Venture{bati} sasa we unabati usiku huu unaenda wapi
Wakati hiyo bati hata soda tu hupati
Bora huweke kesho unywee chai na chapati
Asiye na kitu mi naona bora akabaki
Tusije mbele tukashikana mashati
Suka eh! tuanzie Masaki
Mchizi kapiga simu yaani kuna bonge la party

Rudia kiitikio x2

Verse:- III Ngwea
Dereva funga break tushafika kwenye party

:-MOX

{Eeeh bwana eh kumbe bonge la party}

 :-NGWEA
Cheki mademu kibao utadhani kitchen party..

:-MOX

{Duh!cheki lile anti lililovaa skintight
Ee bwanaeh!liko safi sio mchezo babake unaweza ukahonga laki

:-NGWEA

{Aah wapi mtu kama mi hanipati
Usawa wenyewe huu wa kulenga kwa manati}

:-MOX

Poa basi tujichanganye katikati
Tukacheki mitungi na mademu wa mikasi

Bridge
Braza mwenye black unaitwa na yule anti
’Yuko wapi’
yule aliyevaa suti ya kaki
Anti vipi?

(Rah P)
Aah safi samahani kwa kukupotezea wakati
Nilikuwa naomba tuwe wote kwenye party
Au unasemaje?:

(Ngwea)
Mi naona safi

(Mchizi Mox)
Samahani wewe anti ambaye umevaa shati
Hivi unaitwa nani eh?}:naitwa Bahati:
Hivi anti nishawahi kukuona wapi?

(Rah P)
Acha longolongo we sema una sh’ngapi
Oyaa we vipi mpango wako vipi?

(Mchizi Mox)
Mbona mi mazee mpango wangu safi
Ishakuwa usiku twenzetu tukachukue tax
Twenzetu tukapige mikasi

Rudia kiitikio x2

Verse:- IV
Eebwana eh niko arround mazee
Rudia kiitio x2

Na hii nayo...
Gheto Langu

Mangudu Digi...
Dark Master
Ngwair!
Cowboys in the House!

Maseeeela, {Maheeela}
Cowboys in the House!
Maseeeela, {Maheeela}
C'mon, Cowboys in the...

chorus
Maseeela!

Nipeni, nipeni dili masela,
Nipeni dili nikamate mahela, maseela
Nipeni, nipeni dili masela,
Nipeni dili nikamate mahela, maseela
Nipeni dili masela, Maheeela
Nikamate Mahela, Maseela
Nipeni, nipeni dili masela,
Nipeni dili nikamate mahela

yo!
Mtoto wa kiume najituma na nguvu tena jasiri hata shule skusoma skuwa na hela skuwa na akili so...
Nipe dili mbili kila alfajiri then.. then usinipe zaidi ya wiki mbili
usiponiona ujue nishatambaa nishasafiri yaaani... niko mbele mi nasaka mahela
Nipeni, nipeni dili masela, Nipeni dili mi nikamate mahela..maheela
Nicheke, Hata bar zetu ni za vichochoroni, usishangae tukishindia komoni
tunapenda sana ma wine ma champagne, lakini ndo vile tena hatuna mahela!
Tunatamani mamisosi ya kumwaga, ni ma'Pizza ma'Burgers na Mazagamazaga, {Zaga!}
Ila ndo vile tena hatuna mahela, leo wenyewe ma'cowboy wameshindia Mapera
Tumekondeana kama miili ya Misumari, si unajua kuwa mwili huwa haujengwi kwa tofali
Bali kwa ugali wa maharage au Pizza pepperoni, au kitu cha Beef then mixer Macaroni
Inapendeza ni mambo tu ya fedha, full diet ni muhimu ipatikane kwa meza {mh!}
So, nyie mnasemaje masela, tusake dili tukamate mahela, riight

chorus
Maseeela!

Nipeni, nipeni dili masela,
Nipeni dili nikamate mahela, maseela
Nipeni, nipeni dili masela,
Nipeni dili nikamate mahela, maseela
Nipeni dili masela, Maheeela
Nikamate Mahela, Maseela
Nipeni, nipeni dili masela,
Nipeni dili nikamate mahela

yo
Sjui hata nifanye dili ipi, naona kama vile zote hazilipi yaani...
Nishaamua mi kufanya muziki, kuja 41 nae eti anataka mahela
nimeshachoka haya maisha ya mtaani, ofisi maskani, breakfast mjani {of course yes}
wakati kichwa kinawaza mamilion, vipi nita'ride na marque stallion {check bling bling}
So kila kona ya mtaa kujimix, figure dili one two, one two the five six
ikiwezekana unapiga hata fix, so acha uoga wa kulala sjui kituo cha polisi
bila mapene jua mengi utamiss, achia mbali lazima wajinga wata diss
mi mwenyewe mtu fulani wa ma'chicks, vipi nitaopoa miss bila ya kuwa na mahela?
sio visenti kama fifty fifty, kutembea mfukoni mchizi sina hata jiti
so, nyie mnasemaje masela tusake dili tutadaka mahela, yeaaaaaah!

chorus
Maseeela!

Nipeni, nipeni dili masela,
Nipeni dili nikamate mahela, maseela
Nipeni, nipeni dili masela,
Nipeni dili nikamate mahela, maseela
Nipeni dili masela, Maheeela
Nikamate Mahela, Maseela
Nipeni, nipeni dili masela,
Nipeni dili nikamate mahela

na, na
sjui nimcheki freddy, bob waziri au mwanangu zizzou sjui nani anipe dili
tena iwe moja tu yenye akili, ile ya kulala maskini na kuamka tajiri
nipeni dili nami nitoe mashairi yenye akili ili wenye sigiri wote wakiri
na kabla ya vocals ni smoke up bob marley kisha nitoe rhymes zenye sumu kali ka rift valley
na burn copy ka ice cream za Bakhresa, ni'make more money, more dough more pesa {cash}
Na waliozusha, {majombaz wawe teja!} kesha wapange foleni kuja kugombea umeneja {haha}
na wasionipenda ndo wazidi nichukia, ila dada zao kwenye kona sitoacha kuwabambia hola!
au mnasemaje masela na dawa yao ni kupata mahela, nipeni dili

chorus
Maseeela!

Nipeni, nipeni dili masela,
Nipeni dili nikamate mahela, maseela
Nipeni, nipeni dili masela,
Nipeni dili nikamate mahela, maseela
Nipeni dili masela, Maheeela
Nikamate Mahela, Maseela
Nipeni, nipeni dili masela,
Nipeni dili nikamate mahela

Maseela, maheeela
Maseela, maheeela C'mon
Maseela, maheeela Cowboy
Maseela, maheeela
Maseela, maheeela

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates