ASKOFU mkuu wa kanisa katoliki jimbo kuu la
Arusha ,Josaphat Lebulu ameitaka serikali kutoa majibu ya msingi juu ya matukio
ya kigaidi yanayozidi kuyaandama madhehebu ya Kikristo ikiwemo kuuawa kwa
viongozi wa dini na weingien kujeruhiwa pamoja na kuchomwa kwa makanisa .
Kauli hiyo ameitoa katika hospitali ya Mkoa
Mount Meru, wakati alipotembelea majeruhi wa bomu la kurushwa kwa mkono
lililotokea jana wakati wa uzinduzi wa kanisa katoliki la Mtakatifu Joseph
Mfanyakazi lililopo Olasiti jijini hapa,ambapo watu wawili walifariki dunia na
wengene zaidi ya 60 walijeruhiwa.
Alisema kumekuwepo ma mfululizo wa matukio ya
kigaidi yaneyoelekezwa kwa makanisa pamoja na viongozi wa dini lakini serikali
imeshindwa kutoa jibu kuhusiana na wahusiaka wa matukio hayo.
Aidha alisema kanisa halita lipiza kisazi ila
halitaacha kusema juu ya uhalifu huo na kwamba serikali pamoja na vyombo vya dola ikiwemo mahakama ndio wenye mamlaka ya
kuuambia umma chanzo cha matukio hao pamoja na wahusika wa uhalifu huo.
“Wakatoliki hatuna desturi ya kulipa kisasi, najua
hiyo ni kazi ya shetani imewaingia…tamko letu ni hilo hilo alilotoa Yesu Kristo
la kutolipa ovu kwa uovu…ila hatuwezi kukaa kimya na kuruhusu matukio kama haya
yaendelee,” alisema na kuongeza, “kwanini haya yanafanyika? Kwa nini Watanzania
tunauana hovyo?
“Kama ni mwizi anatafuta nini kwa watu wanaosali na
anawatupia bomu, huu ni ugaidi kabisa, sasa nani anayefanya na nani
anayedhamini, ni wajibu wa serikali kutoa majibu wa mambo matukio haya,”
alisema.
Akiongea na vyombo vya habari mkuu wa Jeshi
la Polisi nchini, (IGP), Said Mwema, amesema tukio la kurusha bomu kwenye
mkusanyiko wa waumini lililotokea Jumapili katika Kanisa la Parokia ya
Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Olasiti jijini hapa, halikupangwa na mtu na
kutekelezwa na mtu mmoja pekee yake.
Alisema tukio hilo la kushtua na la aibu
lazima litakuwa limepagwa na watu wengi na kwa uchunguzi unaoendelea kufuatia
kukamatwa kwa watuhumiwa kuna kila uwezekano kuwanasa waliopanga na kuratibu
tukio hilo.
IGP Mwema alisema hayo juzi jioni wakati
akizungumza na wananchi waliofurika kwa wingi kwenda kuwajulia hali majeruhi wa
tukio hilo katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru.
“Ni tukio la kushtua, kusikitisha, tumefika
eneo la tukio na kuona hali halisi, tunashukuru kupata ushirikiano mzuri wa
wananchi, napenda niwaeleze kwamba kuna kila dalili zote za kuwanasa waliopanga
na kuratibu tukio hili.
“Tukio hili sio la mtu mmoja, wapo
waliohusika katika kupanga, kuratibu, kushauri, kuchangia gharama na wale
waliofanikisha. Dalili zinaonyesha tutawajua na kuwanasa waliohusika hivi
karibuni,” alisema.
Akizungumza kwa niaba ya maaskofu wenzake
waliowatembelea majeruhi hospitalini hapo, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa, alisema amesikitishwa sana
na tukio hilo.
Askofu Mkuu Malasusa, pamoja na maaskofu
wenzake walikuwa wameambatana na Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal,
wakitokea mkoani Shinyanga, kwenye uzinduzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania, Dayosisi Kusini Mashariki mwa Ziwa Victoria, na baada ya kusikia
tukio hilo walikuja kuungana na wananchi wa Arusha na kuwapa pole.
Akizungumzia tukio hilo, Makamu wa Rais, Dk
Bilal, alitoa pole kwa waumini, wakazi wa Arusha, majeruhi na ndugu zao na kwa
uongozi wa kanisa, alisema serikali itawasaka wahusika usiku na mchana.
Naye Naibu
waziri wa Mali asili na utalii,Lazaro Nyarandu,pamoja na kutoa pole kwa
majeruhi wa tukio hilo,alitoa msaada wa mablanketi 50 yenye thamani y ash,milioni
2.3 na kuahidi kutoa shilingi milioni 16 zitakazotolewa na mamlaka ya ya
hifadhi Tanapa.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia