Mkurugenzi wa Executive
Solution, Aggrey Mareale (wa kwanza kulia, alivaa mavasi meusi), Mshindi
wa pili, Veronica Chami, mshindi wa Redds Miss Moshi, Winlady White (mwenye
taji), mshindi wa tatu, Ester Freddy na Mgeni Rasmi, Kamanda wa Polisi ACP-Robert
Boaz.
****** ******
Habari na Picha: Fadhili Athumani.
WINLADY WHITE MUSHI (20), Mwanafunzi wa
mwaka wa pili katika biashara, Chuo cha Biashara na Ushirika Moshi (MUCCoBS),
mshiriki namba 1, ametawazwa kuwa malkia mpya wa urembo Moshi mjini, Redds Miss
Moshi 2013.
White mwenye ndoto za kuwa mbunifu wa
kimataifa, huku ikiwa ndio mara yake ya kwanza kushiriki ulimbwende,
alifanikiwa kutwaa taji hilo na kumrithi Redds Miss Moshi 2012, Angela Filbert.
Timu ya majaji watano wakiongozwa na
Jaji mkuu, Jaji Brian walimtawaza Malkia huyo akiwabwaga wapinzani wake,
Veronica Chami, Martha Charles, Winnie Macha na Ester Freddy.
sema kwa kuzingatia vigezo vyote vya
mashindano ya ulimbwende vinavyotumika kitaifa na kimataifa wote kwa pamoja
waliridhika na kila walichokishuhudia kabla ya kuamua kumtangaza Wnlady White
kuwa Redds Miss Moshi mwaka 2013.
Washindi wengine ni, Mshindi wa pili,
Mshiriki namba 9, Veronica Chami, (1st runner up), mshindi wa Tatu,
mshiriki namba 3, Esther Freddy (2nd runner up), mshindi wa 4,
mshiriki namba 15, Martha Charles (3rd runner up) huku nafasi ya
tano ikienda kwa mshiriki namba 13, Winnie Macha (4th runner up).
Adija Ibrahimu, ambaye ni mshiriki
namba 6, alitangazwa kuwa Miss Talent 2013, akimbwaga mpinzani wake wa pekee
mshiriki namba 4, Jacky Mushi ambaye tangu mwanzo wa kinyanganyiro alikuwa
anapigiwa upatu wa kuchomoka na taji hilo.
Burudani la nguvu liliporomoshwa na
Msanii mkongwe wa bongo Fleva, Prince Dully Sykes, akisindikizwa na wasanii
wengine kutoka Moshi na kuwakonga mashabiki waliofurika ukumbini hapo akiwemo,
mgeni rasmi, Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, ACP- Robert Boaz na
Mkurugenzi wa Executive Solution, Aggrey Mareale.
Redds Miss Moshi 2013, yaliyofanyika
katika ukumbi wa Aventure mjini hapa, yalidhaminiwa na Redds Original, Panone
and Company Ltd, Bonite Bottlers, Baba G, A n A Boutique na Zoom net Printers
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia